Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Disemba 27


WAKALA wa Ujenzi wa Barabara Nchini (TANROAD'S) Mkoani Pwani, unafanya tathmini katika eneo litakalotolewa fidia ,ikiwa ni hatua ya matarajio ya kuanza ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Maneromango-Mzenga, Mlandizi hadi Makofia yenye urefu wa km 100.


Ujenzi wa barabara hiyo itakuwa neema kwa wakazi na watumiaji wa barabara kutoka Maneromango -Makofia ,kwani ni hitaji na kilio cha kipindi kirefu.


Meneja wa TANROADS mkoani Pwani, Mhandisi Baraka Mwambage,akizungumzia kuhusiana na zoezi hilo alieleza, wanashirikiana na wananchi katika ukokotoaji wa gharama halisi za fidia kwa kila mmiliki wa eneo na zoezi linakwenda vizuri.


Mwambage alieleza, ni zoezi la uonyeshaji wa aina, idadi na thamani ya mali zilizopo ndani ya eneo linalotegemea kufidiwa.


"Tunaendelea kupokea maoni na kuyawasilisha kwa timu ya wathamini toka Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali, ili changamoto zinazojitokeza ziweze kutolewa ufafanuzi stahiki kwa maandishi," alifafanua Mwambage.


Aliongeza kuwa hatua hiyo itafuatiwa na uwasilishaji wa taarifa sahihi na shirikishi serikalini.


Vilevile Mwambage alitoa wito kwa wananchi wenye maeneo na mali zilizomo kwenye mpango wa fidia, kujitokeza ili kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.


"Hatua hii ya kupokea maoni ama malalamiko ya wamiliki yanalenga ushirikishwaji wa pande zote mbili kati ya TANROAD'S na wananchi wataopitiwa na mradi huu, tunaendelea kupokea maoni yao na kuyatolea ufafanuzi kwa mujibu wa sheria,"


Baadhi ya wananchi wanaopitiwa na mradi , akiwemo Mkweche walielezea kufurahishwa kwao kwa kuelekea kuhitimishwa kwa kitendawili hicho kilichodumu miaka nenda rudi.


"Kila mtu na maono au mtazamo wake, binafsi kiwango nilichofidiwa ni tofauti na kilichofanyika misimu tofauti ya nyuma, isitoshe inaonekana sasa hivi Serikali imedhamiria kumaliza sintofahamu hii," alisema Mkweche.


Wengine wameenda tofauti walilalamikia kuharibika kwa nyumba zao, sambamba na abiria wanaotumia barabara hiyo wakiipa jina la barabara ya uchaguzi.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...