NA DENIS MLOWE, NKASI

HALMASHAURI ya Wilaya Nkasi Mkoani Rukwa Katika kipindi cha mwaka 2022/2023 imepokea zaidi ya shilingi bilioni 13.02 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo ikiwemo ya elimu, afya iliyotolewa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.


Akizungumza na wanahabari , Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali alisema kuwa fedha hizo zimetolewa na Mama Samia Suluhu Hassan ikiwa ni kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo ambayo yote iko katika kiwango cha asilimia 96 na mingine kukamilka wananchi kuona matunda yake.


Alisema kuwa fedha hizo zimetumika kwenye miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu afya, kilimo na mifugo na miradi mingine ya maendeleo ambayo imejengwa katika maeneo ambayo awali yalikuwa hayana kabisa ikiwemo shule za msingi pembezoni mwa wilaya ya Nkasi na nchi jirani.

Lijualikali alisema kuwa Shilingi bilioni 1,535,600,000 zimepokelewa na kufanya kazi ya ujenzi wa shule mpya tatu za msingi za Isaba, Mtakuja na Ntalamila ambapo ujenzi umehusisha vyumba 8 vya madarasa, jengo la utawala, vyumba 2 vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa awali pamoja na ujenzi wa vyoo vya walimu na wanafunzi na kuongeza kuwa fedha hizo zimetumika kujenga vyumba 15 vya madarasa katika shule za msingi za Mtapenda.


Aliongeza kuwa kati Shilingi milioni 200,000,000 zilitumika kwa ajili ya ukamilishaji wa nyumba 8 za walimu katika shule za msingi za Sentamapufi, Mjimwema, Nkata, Lyantwiya, Itanga, Mkiringa, Lwesusi na Lusembwa.Shilingi 180,000,000 zilipokelewa kwa kufanya kazi ya ukarabati wa vyumba 9 vya madarasa katika shule za msingi za Mkwamba, Itete, Kate, Kala, Utinta na Chalantai,Tundu,Mkombe, Kirando na Lupata.


Aidha alisema kuwa fedha nyingine zaidi ya sh.milioni 180 zilitumika katika ujenzi wa ukamirishaji wa maabara sita katika shule sita za Korongwe Beach, Mashete, Sintali, Ninde, Wampembe na Kirando Itete na Shilingi 40,000,000 kwa ajili ya ukamilishaji wa mabweni 2 katika shule mbili za sekondari za Nkasi na Kate ,Shilingi 50,000,000 zimepokelewa na kufanya kazi ya ukamilishaji wa bwalo moja katika shule ya sekondari Nkasi


“Sekta ya elimu tushukuru kwamba Mama samia kaitendea haki katika wilaya yetu ya Nkasi na kuwataka wazazi wawapeleke Watoto wao shule kwani hatapenda kusikia kuna michango ya ada wala madawati kwani kila kitu kipo sawa kwenye shule zetu na zimejengwa shule za kisasa kutokana na fedha za mama samia zilizoletwa kwenye kipindi hiki” alisema

Akizungumzia sekta ya afya alisema kuwa miradi mingi imetekelezwa na serikali chini ya Mama Samia Suluhu Hassan ambapo fedha mbalimbali zimepokelewa na katika wilaya hiyo ikiwemo kiasi cha Shilingi 800,000,000 zimepokelewa na kutumika kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika hospitali ya Wilaya ,Shilingi 200,000,000 zimepokelewa na kufanya kazi ya ukamilishaji wa zahanati katika vijiji vinne.


Aliongeza kuwa Shilingi 659,093,063 fedha za Mfuko wa pamoja wa Afya (HSBF) zimepokelewa Na kufanya kazi ya ufuatiliaji, ununuzi wa dawa, mafunzo pamoja na ukarabati Mdogo wa vituo vya kutolea huduma za afya, shilingi 456,140,548 zimepokelewa na kufanya kazi ya ujenzi wa vyoo bora katika Zahanati za 9 za Utinta, Miombo, Kizumbi, Musilihofu, Mlambo, Mpasa, Kate, Swaila na Lyele na Shilingl 300,132,000 zimepokelewa kwa ajili ya Mitihani kwa wanafunzi wa kidato cha pili na nne.


“Kwa kweli tunamshukuru sana Mh. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutimiza ahadi mbalimbali kwa wananchi wa Nkasi katika sekta ya afya wananchi wanajivunia sana kuwa kiongozi anayewajali kwani sekta ya afya imepokea fedha nyingi zaidi na wanahabari nitawaomba mje kutembelea kujionea wenyewe mambo yaliyofanyika katika wilaya hii.” Alisema LijualikaliS


Lijualikali alisema kuwa kwa kipindi hichi Shilingl 315,523,910 fedha ambazo zlipokelewa za ujenzi wa miundombinu katika vituo vya kutolewa huduma za afya ambavyo ni Kasu, Kate, Nkundi (Kantawa) Londokazi, Korongwe, Mwai, Nkomolo, Kabwe, Mashete na Hospitali ya Wilaya.

“{Kuna fedha nyingi zimeendelea kutolewa na serikali ya Mama Samia kwa ajili ya wananchi wa wilaya hii hivyo napenda kutoa shukrani za dhati kwa Serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Mhe. Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya Maendeleo. Aidha fedha hizi zimesaidia uboreshaji wa utoaji wa huduma za elimu na afya katika vituo vya kutolea huduma pamoja na huduma zingine.Tunaomba Mungu azidi kumlinda siku zote za Maisha yake “ alisema.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...