Na Mwandishi Wetu, Ivory Coast

Golikipa wa Cameroon, André Onana huenda akacheza michezo miwili ndani ya saa 24 akiwa na Klabu ya Manchester United ambayo itacheza dhidi ya Tottenham, Januari 14 na timu ya taifa ya Cameroon ambayo itacheza dhidi ya Guinea, Januari 15 mchezo wa ufunguzi wa Kundi C wa mashindano ya AFCON.


Tovuti ya michezo ya Mirror imeripoti kuwa Man United waliingia mkataba na Shirikisho la Soka nchini Cameroon, kwamba Klabu hiyo kuwa na Onana hadi Januari 14. Maana yake Golikipa huyo atabaki Klabuni hapo kwenye mchezo dhidi ya Wigan na mchezo dhidi ya Tottenham kabla ya kupanda Ndege (masaa saba) kuwahi Ivory Coast kwenye mashindano ya AFCON.


Cameroon watacheza na Guinea kwenye mchezo wao wa ufunguzi wa mashindano hayo ya AFCON, Januari 15 majira ya saa 11 jioni kwa saa za Uingereza, baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza ambao utachezwa Januari 14 kati ya Man United dhidi ya Tottenham majira ya saa 10:30 jioni kwa saa za Uingereza.


Ratiba ya timu ya taifa ya Cameroon ipo hivi; Kikosi hicho chini ya Kocha Mkuu, Rigobert Song baada ya hapo kitacheza dhidi ya Senegal (Januari 19) na kumaliza michezo yake ya Kundi C dhidi ya Gambia (Januari 23).


Pia, kuna uwezekano wa Onana kutokosa mchezo wowote wa Man United akiwa na kwenye mashindano ya AFCON, endapo Cameroon hawataendelea na hatua inayofuata ya mtoano, Onana atakuwepo kwenye Kikosi cha Man United kwenye mashindano ya FA raundi ya nne ambapo watacheza dhidi ya Eastleigh au Newport, Januari 27.


Ndani ya wiki mbili zijazo, Manchester United hawana ratiba yoyote baada ya kucheza dhidi ya Tottenham, Januari 14. Man United watakuwa na mchezo mwingine wa Ligi Kuu (EPL) dhidi ya Wolves, Februari 1.


Endapo Cameroon itafuzu Fainali ya Michuano ya AFCON 2023 nchini Ivory Coast, Fainali ambayo itachezwa Februari 13, Golikipa Onana atalazimika kukosa michezo minne ya Man United ikiwemo mchezo muhimu dhidi ya Aston Villa.


Hata hivyo, Klabu nyingi za Ligi Kuu nchini Uingereza zimewaachia wachezaji wao kwa ajili ya mashindano hayo ya AFCON tangu Januari 1, lakini Man United wanaendelea kuwa na Onana hadi leo Januari 14 kwenye mchezo wao dhidi ya Tottenham.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...