Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amefanya ziara katika chanzo cha maji cha Ihelele kilichopo Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza ikiwa ni Mradi mkubwa wa kimkakati wenye thamani zaidi ya Bilion 900 na kuendeshwa na Tasisii chini ya Wizara ya Maji ya KASHWASA Chanzo hiki cha Ziwa Victoria kinahudumia mikoa sita na Mamlaka za Maji nane(8) ambazo ni SHINYANGA, KAHAMA, MAGANZO TABORA, NZEGA, IGUNGA, KISHAPU na MWAUWSA-NGUDU.

Katika ziara hiyo Waziri Aweso ameeleza kutoridhishwa na uendeshaji na utendaji kazi wa Mamlaka ya Maji KASHWASA kutokana na kuwepo kwa changamoto mbalimbali za uendeshaji ikiwa ni pamoja na upungufu wa madawa ya kutibu na kusafisha Maji akimtaka Mkurugenzi wa KASHWASA Eng Patrick Zamba na Menejimenti yake kujitathmini na kueleza kwamba hatosita kuchukua hatua hali ya utendaji kazi isipobadilika haraka.

Akizungumza na wakurugenzi watendaji wa Mamlaka za Maji nane zinazonufaika na chanzo cha Iherere amewataka Wakurugenzi wote wa Mamlaka za maji nchini kuacha visingizio na kuwajibika ipasavyo kutimiza majukumu yao ya kiutendaji ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya maji safi na salama wakati wote na kuendesha mamlaka za Maji kwa mafanikio.

Katika hatua nyingine Waziri Aweso amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof.Jamali Katundu kufanya Tathimini ya Mamlaka zote za maji nchini ili kubaini mwenendo wa madeni na madai na kuelekeza aipate taarifa hiyo ndani ya kipindi cha wiki moja


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...