Na Mwandishi Wetu, Hispania

BALOZI wa Tanzania nchini Uhispania mwenye makazi yake jijini Paris, kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya mazungumzo na mashirika makubwa ya ndege yanayofanya safari zao ndani na nje ya bara la Ulaya.

Mashirika hayo ni Air Europa, Iberia, Plusultra na W2M yote ya Uhispania. Aidha, alikutana na Bw. Rosa, mwenye kampuni inayoratibu ndege maalum (charter flights) za kitalii kutoka Lisbon.

Madhumuni ya mazungumzo hayo ni kujadili mipango ya kuanzisha safari za moja kwa moja kati ya miji mikubwa ya Uhispania na Ureno na miji ya Tanzania ili kurahisisha usafiri na kuimarisha utalii.

Balozi Ali Mwadini akiagana na Meneja Masoko wa Kampuni ya ndege ya Plusultra Lineas aƩreas ya nchini Uhispania ambayo ina nia ya kuanza safari barani Afrika.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...