BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imewahimiza wananchi kupeleka sarafu kwenye mabenki ya biashara yaliyo karibu nao.

Akizungumza leo Januari 9, 2024 wakati wa semina iliyoandaliwa na BoT kwa Wahariri wa vyombo vya habari Meneja wa Sarafu, BoT, Ilulu Said amesema kwa sasa kampeni ya ukusanyaji sarafu inahusisha shilingi 50, 100 na 200.

“Sarafu za Tanzania zinakaa miaka 30 bila ya kuharibika kulingana na utunzaji wake, hivyo tunawahimiza wananchi wasikae na sarafu kwenye vibubu, wazipeleke kwenye mabenki wakazi- deposit au wakazibadilishe wapatiwe noti, ili hatimaye ziweze kuwafikia watumiaji wengine kwenye mzunguko wa fedha.”

Ilulu amesema Desemba 2023, BoT iliyaelekeza mabenki yote ya biashara yaanze kupokea sarafu kutoka kwa wnanachi kama desposit, lakini pia hata kwa wananchi ambao hawana akaunti kwenye benki hizo nao wako huru kupeleka sarafu na kubadilishiwa ili wapewe noti.

Ameongeza kwamba katika kampeni hiyo wameondoa vikwazo vya upokeaji wa sarafu hizo, kwani awali walielekeza sarafu chafu ndio zipelekwe kwenye mabenki, lakini kwa sasa benki zimeelekezwa kupokea sarafu zote, chafu na safi.

Ilulu alitoa maelezo hayo kwa kina wakati wa semina hiyo ya siku moja kuhusu Mfumo Mpya wa Uandaaji wa Sera ya Fedha (Interest Rate-Based Monetary Policy Framework) na Ukusanyaji wa Sarafu.



Meneja wa Sarafu, BoT, Ilulu Said

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...