Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

SHULE ya Feza imesema kwamba kutokana na juhudi za serikali kuboresha shule zake imekuwa chachu kwako kuendelea kujenga miundombinu msingi ya ufundishaji taaluma ili kuchochea maendeleo ya elimu hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo asubuhi , Shabani Mbonde Msaidizi wa Mkuu wa Shule Taaluma, amesema kwamba kutokana na uboreshaji unaofanywa na serikali kupitia shule zake imewalazimu uongozi wa shule ya Feza kuendelea na maboresho ya miundombinu yake ambayo imefanya kuweza kupata matokeo mazuri ya kidato cha nne mwaka huu .

Amesema kwamba matokeo ya mwaka huu ya kidato cha nne shule hiyo ya Feza ambayo ni moja ya shule bora za sekondari hapa nchini imeweza kupata kufaulisha wanafunzi wote wa kidato cha nne kwa daraja la kwanza wanafunzi 76

“Wanafunzi wetu wote 76 wa kidato cha nne mwaka huu wamepata daraja la kwanza (Division 1 ) kati yao wanafunzi 47 wamepata daraja la kwanza kwa pointi 7 (Division 1 .7) huu ni Ushahidi tosha kwamba shule bado ni kituo bora cha taaluma hapa nchini,’ Aliongeza Mbonde

Aliongeza kwamba shule hiyo ya Feza itaendelea kuboresha miundombinu yake ya elimu ili kukuza vipaji na kuweka mazingira mazuri kwa mtoto yoyote wa kitanzania anayepitia shule hiyo anaweza kufaulu na kuwa mtu bora kwa familia yake, jamii na nchini kwa ujumla.

Mbonde alisisitiza pia kwamba shule yao ya Feza ina mazingira Rafiki kwa mwanafunzi kuanzia ufundishaji , vifaa , maabara , maktaba na kila darasa lina wanafunzi wasiozidi 25 ili kumwezesha mwalimu kuweza kutambua kila mwanafunzi na kutoa msaada wa karibu pale inapohitajika.

“shule yetu ya Feza itaendelea kupambana na kupambanua wigo wa ufundishaji kwa kuhakikisha kwamba kila mwanafunzi anapewa mazingira bora katika utoaji wa elimu ili kuwasaidia vijana wetu kufikia malengo yao ya kielimu,” alisema

Kwa upande wake, Naibu Mkuu wa Shule , Richard Maina amesema kwamba shule yao imeweza kufaulisha wanafunzi wote 76 wa daraja la kwanza kutokana na ushirikiano mkubwa wanaopata kutoka kwa wazazi  na wadau wengine wa elimu hapa nchini.

Alisisitiza kwamba kufaulisha kwa kiwango hicho ni utamaduni wao wa muda tangu shule hiyo ilipoanzishwa miaka 25 iliyopita kwa kutumia programu ya ana kwa ana yaani kila mwanafunzi anapata nafasi ya kukaa na mwalimu ili aweze kupata msaada wa kipekee katika taaluma.

“Hayo matokeo ya jana ya kidato cha nne kwa shule yetu ni ishara kwamba utatu mtakatifu wa ushirikiano kati ya mwalimu , mzazi na mwanafunzi ndio kichocheo kikubwa katika kupata matokeo haya chanya kwa shule yetu,” alisema

Aliongeza kwamba shule hiyo ya Feza inapenda kutoa shukrani za pekee kwa wadau wa elimu hapa nchini kuanzia ngazi ya Taifa, Mkoa , Wilaya na kata na Baraza la Mitihani ya Taifa kwa ushirikiano mkubwa wanaotoa kwao,

“pia napenda kuchukua nafasi kuwashukuru wafanyakazi wote wa shule ya Feza wavulana na wasichana , wafanyakazi , uongozi na wazazi kwa wadau muhimu wa maendeleo ya shule hiyo hapa nchini na Feza ni sehemu sahihi kwa mtoto wa kike na kiume kusoma hapa nchini,” aliongeza

a mazingira mazuri ya ufundishaji na ujenzi ya miundombinu msingi wa elimu ambayo imewawezesha kupata matoke ohayo.

“Hayo matokeo tuliyopata inatokana na juhudi zetu zote kati ya walimu , wazazi na sisi wanafunzi pamoja na sala ndio siri pekee ya shule yetu kuendelea kutoa matokeo mazuri,” alisema

Asna Ali (17) ambaye ni mhitimu pia wa kidato cha nne aliyepata daraja la kwanza (Division 1.7) alisema kwamba juhudi kubwa za walimu katika kuwajenga kitaaluma, kinidhamu na malezi bora ni kichocheo cha kuendelea kufanya vizuri kwa shule kwenye matokeo ya kidato cha nne hapa nchini.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...