Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Naghenjwa Kaboyoko akichangia hoja baada ya wasilisho la taarifa ya programu ya kukuza ujuzi wa nguvu kazi nchini inayotekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika leo Januari 24, 2024 Bungeni jijini Dodoma.

Na, Mwandishi Wetu - DODOMA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imepokea taarifa ya Programu ya kukuza Ujuzi wa Nguvu Kazi nchini inayotekelezwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Naghenjwa Kaboyoka akizungumza leo Januari 24, 2024 baada ya kupitia na kuchambua wasilisho la Ofisi hiyo Fungu 65 kuhusu programu hiyo, amesema wasilisho hilo litasaidia kamati kutoa ushauri utakaoongeza ufanisi kwenye utekelezaji wake wa kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira.

Akijibu hoja za wajumbe wa kamati hiyo, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mhandisi Cyprian Luhemeja, amesema serikali imeendelea kutanua wigo wa ukuzaji ujuzi kwa vijana na hadi sasa wamenufaika 141,968 kupitia programu ya kukuza ujuzi iliyoanza kutekelezwa Mwaka 2016/17.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakifuatilia wasilisho la taarifa ya Programu ya kukuza ujuzi wa nguvu kazi nchini inayotekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu wakati wa kikao cha kamati hiyo cha kupokea taarifa hiyo Kilichofanyika leo tarehe 24 Januari, 2024 Bungeni jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Naghenjwa Kaboyoko akichangia hoja baada ya wasilisho la taarifa ya programu ya kukuza ujuzi wa nguvu kazi nchini inayotekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika leo Januari 24, 2024 Bungeni jijini Dodoma.

Mkurugenzi Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ally Msaki akiwasilisha taarifa ya programu ya kukuza ujuzi wa nguvu kazi nchini inayotekelezwa na ofisi hiyo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) cha kutoa taarifa ya programu ya kukuza ujuzi wa nguvu kazi nchini kilichofanyika leo Januari 24, 2024 Bungeni jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa ufafanuzi wa hoja zilizowasilishwa na wajumbe wakati wa kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) cha kutoa taarifa ya programu ya kukuza ujuzi wa nguvu kazi nchini inayotekelezwa na ofisi hiyo kilichofanyika leo tarehe 24 Januari, 2024 Bungeni jijini Dodoma

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...