Na. Omar Hassan, Said Bakari – ZANZIBAR

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Hamad Khamis Hamad amesema upatikanaji wa vifaa vya kisasa katika Jeshi la Polisi kunachangia mageuzi makubwa ya matumizi ya teknolojia katika utendaji kazi na kudumisha ustawi na usalama wa raia na mali zao. 

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Kumpyuta kumi na tatu (13) kutoka katika kampuni ya ASAS GROUP alisema vifaa hivyo vitaliwezesha Jeshi la Polisi kutoa huduma bora na kwa wakati kwa kutatua changamoto mbalimbali za uhalifu na wahalifu.

Nae Mwakilishi kutoka ASAS GROUP Fahad Masoud Ali alisema Kampuni hiyo imetoa vifaa hivyo kwa Jeshi la Polisi ili Jeshi hilo liendelee kusimamia Amani na usalama uliopo na pia wanaunga mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussen Ali Mwinyi, za kuleta Maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...