SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Tulia Ackson (Mb) leo Januari 25, 2024 amewashukuru uongozi wa Mtandao wa wanawake wa Jeshi la Magereza Kwa kumpongeza Kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa 31 na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani kwa kuchaguliwa katika kikao cha Baraza la Uongozi kilichofanyika Oktoba 23- 27 , 2023 Jijini Luanda nchini Angola na kuwa Rais wa tatu mwanamke na Rais wa kwanza mwanamke kutoka Barani Afrika, shukrani hizo amezitoa katika Ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.

Aidha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumpigia kampeni na hatimae kushinda na kuchaguliwa kuwa Rais wa Jumuia ya Mabunge Duniani.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa wanawake wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza Elizabeth Mbezi akiongea Kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Mzee Ramadhani Nyamka na kwa niaba ya Mtandao wa wanawake wa Jeshi la Magereza amesema kuwa tuzo hiyo ni maalumu ya kumpongeza na kumuonyesha kuwa Mtandao huo wa Wanawake wa Jeshi la Magereza upo na unamuunga mkono katika kutimiza majukumu yake katika maendeleo ya Tanzania kwa ujumla.

Amesema kuwa kuipata nafasi hii ya Urais wa Jumuia ya Mabunge Duniani umeipa Taifa letu la Tanzania heshima kubwa hasa ukizingatia kuna nchi nyingi zilizo endelea kisayansi na kiteknolojia zingeweza kuchukua nafasi hiyo.

Ameongeza kuwa mtandao wa wanawake wa Jeshi la Magereza unampongeza sana na umeahidi kushirikiana vilivyo katika shughuli mbalimbali katika maendeleo ya jamii na taifa Kwa ujumla.
.Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akipokea tuzo ya pongezi ya kuchaguliwa kuwa Rais wa umoja wa Mabunge Duniani kutoka Kwa Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa wanawake wa Jeshi la Magereza ACP.Elizabeth Mbezi.
 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson katikati akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mtandao wa wanawake wa Jeshi la Magereza katika Ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es salaam.
 

Mtendaji wa Mtandao wa wanawake wa Jeshi la Magereza Asp. Oliva Kilambo akimpa mkono wa pongezi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Tulia Ackson katika ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...