Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Mhe. Haroun Ali Suleiman amewataka wanachama wa chama cha Mapinduzi kuendeleza mashirikiano katika kudumisha Amani na utulivu uliopo nchini ili kujiletea Maendeleo ya haraka.
Ameyasema hayo huko Makunduchi Wilaya ya kusini alipokuwa akifunga mafunzo ya madarasa ya itikadi katika tawi la Muyuni A, Kajengwa B na Miwaleni Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema mashirikiano ya pamoja yatakiwezesha Chama hicho (CCM) kuendelea kupata ushindi katika uchaguzi mkuu wa Raisi, wabunge, wawakilishi na madiwani, unaotarajiwa kufanyika mwakani 2025.


Aidha amewataka vijana hao kuwa wazalendo na kuhakikisha wanayafanyia kazi mafunzo waliopatiwa ili kuleta tija kwao, pamoja na kukiletea maslahi Chama hicho na taifa kwa ujumla.


Pia aliwataka kuendelea kunadi na kuhamasisha sera za Chama Cha Mapinduzi kwani Ilani ya Chama hicho inatilia mkazo maendeleo ya vijana katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuwawezesha kuzifikia fursa ajira zitokanazo na uchumi wa buluu.


Mbali na hayo amewapongeza wahitimu hao kwa kuonyesha moyo wa kujitolea katika kipindi chote cha mafunzo ambapo jumla ya vijana 236 walihitimu mafunzo hayo.

Awali aliwapongeza vijana hao kwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuweza kupata haki yao ya msingi ya kuchaguwa na kuchaguliwa.

Nao washiriki wa mafunzo hayo wameahidi kuyafanyia kazi kwa vitendo ili kufikia malengo ya kuendelea kukipatia ushindi chama cha Mapinduzi ifikapo 2025.

Wakati huohuo, Mwalimu Haroun aliwatembelea na kuwafariji wananchi waliothirika na upepo ulitokea January 20 mwaka huu katika baadhi ya maeneo ya jimbo lake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...