Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi mdogo wa China Mhe. Zhang Zhisheng anayefanyia kazi zake Zanzibar, kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa utumishi nchini tarehe :29 Januari 2024, Ikulu Zanzibar.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amemshukuru Balozi Mhe.Zhang Zhisheng kwa kudumisha na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Zanzibar na China katika miaka mitatu ya utumishi wake nchini, pia kwa kuratibu vema ziara yake mwaka jana China.

Vilevile Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa China imeendelea kusaidia Zanzibar na kushirikiana katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya kwa kuleta madaktari kutoka China, ufadhili wa masomo, kujengea uwezo, biashara, utalii, pamoja na kuwepo kwa kampuni za kichina katika kazi za miradi mbalimbali ya miundombinu ya barabara, bandari, na uwanja wa ndege.

Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi amewakaribisha wawekezaji kutoka China kwenye sekta ya utalii kujenga hoteli kwa kuongeza watalii zaidi wa Kichina kuitembelea Zanzibar.

Rais Dk.Mwinyi amesema Zanzibar itaendelea kushirikiana na kudumisha uhusiano na China ambayo yametimiza miaka 60.

Naye Balozi Mhe.Zhang Zhisheng amesema China itaendelea kushirikiana na Zanzibar kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...