Leo tarehe 17 Januari, 2024. nimekutana na kufanya mazungumzo na Ndugu Craig Hart, Mkurugenzi mkazi mpya wa shirika la maendeleo ya Kimataifa la serikali ya Marekani (USAID) katika ofisi za Wizara ya Maji Mtumba Mji wa Serikali Dodoma.

Lengo la kikao ni kujadili ushirikiano kati ya Serikali ya Marekani na Serikali ya Tanzania katika sekta ya Maji.

Aidha Katika kikao nimeishukuru serikali ya Marekani kwa ushirikiano inautoa katika sekta ya maji na kuahidi kuendeleza zaidi mashirikiano hayo.

Zaidi nimesisitiza kuwa Sekta ya Maji ni sekta muhimu sana na hivyo uwekezaji kama huu una tija kubwa kwa watanzania.

Naye Ndugu Hart, amesema Serikali ya Marekani itaendelea kushirikiana na wizara ya Maji na kwamba Serikali ya Marekani imeiweka Tanzania katika mpango maalumu wa mashirikiano ya sekta ya maji, na kiasi cha dollar million 100 zimewekezwa na kutengwa katika sekta ya maji.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...