Safina Sarwatt, Kilimanjaro,

WAPAGAZI ambao wanafanya kazi ya kubeba mizigo ya watalii katika Mlima Kilimanjaro maarufu kwa jina la Wagumu wameuanza mwaka wa 2024 kwa kicheko baada ya mishahara yao kuongezwa.

Akizugumza leo Januari 4, 2024 Mjini  Moshi  mkoani Kilimanjaro, Ofisa kutoka Chama cha Wapagazi Tanzania (TPO) Loishiye Mollel amesema mshahara wao umepanda kutoka Sh.20, 000 ya awali hadi 25, 000.

Amesema kupanda kwa mshahara huo wa wapagazi unatokana na harakati za muda mrefu zilizokuwa zinafanywa na TPO kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania (TATO) Idara ya Kazi  pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Amesema mwaka 2008 kwa maana ya miaka 15 iliyopota, Serikali kupitia Tangazo ya Serikali(GN22)ilipandisha mishahara ya Wagumu na kufikia dola 10 kwa siku lakini zipo baadhi ya kampuni za wakala wa utalii walikuwa wanalipa  chini ya dola 10 kama ilivyopitishwa na Bunge.

Amefafanua tangu wakati huo wagumu hao wamepitia chnagamoto nyingi licha ya kufanyakazi ngumu ya kubeba mizigo yenye uzito wa kilo 20 kutoka lango la kupandia kadi juu haijarishi nyakati za masika ama nyakati za kiangazi .

Aidha Mawaziri kadhaa wenye dhamana na utalii wamepita bila jambo la vijana hao kupatiwa ufumbuzi na mwaka 2015 mapambano ya kudai nyongeza ya mshabara yalipamba moto kwa usaidizi wa TATO, Idara ya Kazi,TRA pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Loishiye Lenoy Mollel kutoka Chama cha wapagazi Tanzania(TPO) ndiye aliyetoa tangazo la kupanda kwa mishahara hiyo kuanzia Januari mosi mwaka huu kwa mgumu kulipwa 25,000 kwa siku na malipo hayo yatadumu kwa muda wa mwaka mmoja na kuanzia Januari Mosi 2025 mishara hiyo itapanda tena hadi kufikia sh,35,000 kwa siku .

Amesema hiyo ni habari njema kwa vijana hao ambao hakika malipo yao hayaendani na kazi ngumu wanayoifanya ndani ya hifadhi ya Taifa ya mlima Kilimanjaro na hup ni mwanzo wa mabadiliko ya michakato mingine ikiwamo suala la mavazi ya kukabiliana na baridi kali ndani ya hifadhi.

"Katika kuhakikisha malipo hayo yanafanyika bila usumbufu kila Mgumu atalazimika kuwa na namba ya utambulisho wa mlipa kodi(TIN) itakayomwezesha kufungua akaunti benki na mishahara yao italipwa na wakala kupitia benki."

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa TATO Sirili Akko amesema ni jukumu la Wagumu kulinda heshima yao kwa kutokukubali kulipwa ujira chini ya viwango vilivyoidhinishwa , kwani  kufanya hivyo ni kuwahujumu wenzao pamoja na mapato ya Serikali .

Ameongeza katika suala la ulinzi na usalama kwa mali za watalii ni mkubwa huku akisisitiza wataeneelea kuuweka katika hali ya usafi Mlima Kilimanjaro ili kuendelea kuwavutia wageni .

 Wakati huo huo baadhi ya Wapagazi wameiomba TATO kuwadhibiti mawakala utalii wanaoendesha kampuni zao mifukoni ambao wamekuwa chanzo cha kuwapa malipo duni huku baadhi yakidaiwa kununua vocha kwa mawakala wenye leseni ya mlimani (TALA).

"Tuna kesi nyingi sana idara ya kazi zinazohusu malalamiko ya mawakala wanaowalaghai Wapagazi,hatuwezi kuboresha utalii kama tunawalaghai, " amesema  Katibu wa KPA Salmin Kerangwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...