Na Ali Issa Maelezo 16/1/2024

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Abdull Mwita amesema Uwanja wa New Aman complex tayari umeshakaguliwa na Viongozi wa FIFA na AFCON Kwa matayarisho ya Mashindano AFCON kwa vijana wa chini ya umri wa miaka 17.


Hayo ameyasema leo huko uwanja New Aman Comlex wakati wa mapokezi ya viongozi wa kamati ya NEC ya chama cha Mapinduzi waliofika kiwanjani hapo kufuatia ziara walioifanya kukagua miradi mbali ikiwemo kiwanja cha New Aman Coplex.

Amesema Uwanja huo utatumika kufuatia ushirikiano wa viongozi wa kuu wa Tanzania Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussen Ali Mwinyi ambapo kwa sasa Uwanja Huo umeshaamuliwa kutumika kwenye michuano hiyo ambapo tayari viongozi wa FIFA na Viongozi AFCON wameshakikagua na wamejirizisha kufanyika michuano hiyo hapa Zanzibar.


Amesema Zanzibar itakuwa mwenyeji wa michuano hiyo jambo ambalo ni jema hivyo kuna kila sababu ya kuwapongeza Viongozi wao kwani ni dhahiri kuwa michuano hiyo itasaidia kuwainua vijana kimichezo na kujipatia ajira kutokana na vipaji vyao.

Nae Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbea na Mjumbe wa NEC alishukuru Serikali zote mbili kwa ushirikiano wao kuona kuwa viongozi hao wapo pamoja kwa kushauriana na kupitisha maamuzi ya busara ya pamoja yanayowaletea maendeleo Wananchi.

Amesema wamekuja kujionea wao wenyewe kukagua miradi mbali iliopitishwa katika ilani ya CCM na kuona kuwa viongozi wao wameikamilisha kwa vitendo ikiwa na ubora wa hali ya juu.


Amesema uwanja wa New Amani Coplex upo katika hadhi ya kimataifa na umekidhi viwango vyote vya kimataifa jambo ambalo ni muelekeo wa wazi kuwa Zanzibar imepiga hatua kubwa katika safu ya michezo kushirikisha mashindano mbali mbali ya kimataifa.


Amesema kutokana na hali hiyo hakuna budi kuwashukuru viongozi wao wa kitaifa kuikamilisha ilani ya CCM pamoja na kumshukuru Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na michezo Tabia Abdull Mwita Kwa usimamizi wa Uwanja huo na kumsaidia Rais wa Zanzibar kwa kumpa ushirikiano kwa kila hatua.


Msafara huo wa wajumbe zaidi ya 30 kutoka NEC umetembelea maeneo mbali ya uwanja huo ikiwemo viwanja vya mpira wa mikono, mpira wa miguu na miungombinu mbalimbali ya uwanja huo.
 

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akiwa na  Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM NEC  akiwatembeza katika Uwanja wa Kimataifa wa New Amani Complex kufuatia ziara maalum ya Wajumbe hao kuangalia Miradi mbalimbali ya Ilani ya Chama hicho  Zanzibar.
 

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita  akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM NEC  baada ya  kuwatembeza katika Uwanja wa Kimataifa wa New Amani Complex kufuatia ziara maalum ya Wajumbe hao kuangalia Miradi mbalimbali ya Ilani ya Chama hicho  Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...