Na Muhidin Amri, Mbinga


ZAIDI ya wakazi 3,852 wa kijiji cha Zomba na Tanga wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma,wameondokana na adha ya maji safi na salama baada ya wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji ya bomba uliogharimu Sh.milioni 817,492,458.


Mhandisi wa maji kutoka ofisi ya meneja wa Ruwasa wilaya ya Mbinga Mhandisi David Charles alisema,ujenzi wa mradi huo umehusisha ukarabati wa chanzo,ulazaji wa bomba kuu na bomba la usambazaji maji umbali wa kilomita 26.617,ujenzi wa vituo 27 vya kuchotea maji na ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji la lita 150,000.


Alisema,kazi zote zilizopangwa kutekelezwa zimefanyika kwa zaidi ya asilimia 98 na fedha zilizotumika hadi sasa ni Sh.milioni 459,130,144 sawa na asilimia 56 ya fedha zilizopangwa kutumika katika kazi hiyo.


Naye meneja wa Ruwasa wilaya ya Mbinga Mhandisi Mashaka Sinkala alisema,wilaya ya Mbinga ina jumla ya vijiji 166 kati ya hivyo vijiji 107 vimefikiwa na huduma ya maji ya bomba na vijiji 59 bado havijapata huduma ya maji ya bomba.


Alisema,kwa mwaka wa fedha 2022/2023 wilaya ya Mbinga ilitengewa jumla ya Sh.bilioni 3.2 kwa ajili ya kutekeleza jumla ya miradi 12,kati ya hiyo miradi 9 imetekelezwa na inatoa huduma ya maji kwa wananchi na miradi 3 haijakamilika na ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.


Alisema,kwa mwaka wa fedha 2023/2024 wametengewa jumla ya Sh.bilioni 5.2 ili kutekeleza miradi 7 ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake na miradi 4 imekabidhiwa kwa wakandarasi na wanaendelea na utekelezaji.


Aidha alieleza kuwa,kabla ya Ruwasa haijaanzishwa mwaka 2019 upatikanaji wa huduma ya maji katika wilaya hiyo ilikuwa asilimia 49.6 na hadi mwezi Disemba mwaka 2023 imefikia asilimia 62 sawa na ongezeko la asilimia 13 katika kipindi cha miaka mitatu.


“Ruwasa tumepiga hatua kubwa sana ya katika kutoa huduma ya maji kwa upande wa vijijini na mategemeo yetu ifikapo mwezi Disemba mwaka huu kati ya vijiji 59 vilivyobaki,vijiji 37 vitakwenda kupata huduma ya maji”alisema Sinkala.


Kwa mujibu wa Sinkala,Ruwasa wilaya ya Mbinga imejipanga kuhakikisha vijiji vingine 22 vilivyobaki vinakwenda kupata huduma ya maji safi na salama ifikapo mwaka 2025.


Mwenyekiti wa chombo cha watumia maji ngazi ya jamii(CBWSO)kijiji cha Tanga Joseph Ndunguru alisema,awali katika kijiji hicho kulikuwa na mradi wa maji uliojengwa tangu mwaka 1970,hata hivyo miundombinu yake ilianza kuchakaa na kushindwa kutoa huduma ya uhakika.


Ameishukuru serikali kupitia Ruwasa,kutekeleza mradi huo ambao umewezesha kupata maji ya uhakika na hivyo kumaliza changamoto ya kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta maji kwenye mito na mabonde ambayo maji yake siyo safi na salama.

 

Baadhi ya wanawake wa kijiji cha Tanga Halmashauri ya Mji Mbinga,wakichota maji katika moja ya vituo vilivyojengwa na wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)wilayani humo.
 

Mhandisi wa maji kutoka ofisi ya meneja wa Ruwasa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma David Charles kushoto,akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Tanga ulianza kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi takribani 3,852 wa kijiji cha Tanga na Zomba.
 

Tenki lenye uwezo wa kuhifadhi lita 150,000 za maji linalohudumia wakazi wa kijiji cha Tanga na Zomba wilayani Mbinga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...