Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema waananchi wa Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi wamejipambanua kwa kutoa shukrani kwa kufanya kazi kuhakikisha Ilani ya Uchaguzi inatekelezeka, kukisemea Chama Cha Mapinduzi (CCM), serikali pamoja na kuzungumza mambo mazuri yanayofanywa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Wilaya ya Ruangwa mbele ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulharman Kinana, pamoja na wananchi wa Ruangwa, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Rais Dk. Samia ameliwezesha taifa kuwa na utulivu.

Pia, amesema chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia nchi imeendelea kuwa na amani pamoja na kuongezeka kwa kasi ya maendeleo huku akifafanua kuwa Rais Samia ameendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ambayo ni ya kimkakati ukiwemo ujenzi bwawa la Mwalimu Nyerere ambalo Februari mwaka huu sehemu ya mitambo yake itaanza kufanya kazi ya kuzalisha umeme.

Waziri Mkuu Majaliwa ameongeza Rais Dk. Samia ameendelea na ujenzi wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) sambamba na kuendelea kuboresha sekta ya afya katika maeneo mbalimbali kwa kujenga miundombinu ya afya, ununuzi wa dawa na vifaa tiba.

Pia, amesema chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan sekta ya elimu imeendelea kuboreshwa kwa ujenzi wa miundombinu ya madarasa kwa shule za msingi na sekondari.

Waziri Mkuu amesema Dk. Samia katika wilaya hiyo amefanya mambo makubwa KWa maendeleo ya wananchi wa Ruangwa akitolea mfano uwepo wa mradi wa maji kutoka Nangawa kuja Ruangwa.

“Wananchi wa Ruangwa tutafanya kazi usiku na mchana, wakati wa jua kali na wakati wa mvua kali kuhakikisha tunamsaidia Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ili atekeleze yale ambayo amepanga kuyafanya kwa Watanzania,”.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...