Na Mwandishi Wetu.

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amesema taarifa za tafiti wa Demographia ya Afya ya Uzazi na Viashiria vya Malaria (TDHS/MIS) ya mwaka 2022 zinaonesha kuwa nchi yetu imepiga hatua katika viashiria vingi vya afya ya mama na mtoto. 

Akizungumza leo Januari 5, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa usambazaji wa vifaa vya kuboresha huduma za afya ya uzazi,  mama na mtoto Waziri Ummy amesema Serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vitakanavyo na uzazi.

"Kwa mfano vifo vitokanavyo na uzazi vimeshuka kutoka 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2015/16 hadi 104 kwa kila vizazi hai 100,000 na vifo vya Watoto chini ya miaka mitano vimeshuka kutoka 67 kati ya vizazi hai 1000 mwaka 2015/16 hadi 43 kwa kila vizazi hai 1000.

"Hii ni sawa na kupunguza vifo vya kinamama wajawazito kutoka 11,000 hadi vifo 2,500 kwa mwaka. Hizi ni jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wadau wa afya ...

"Katika katika kuhakikisha kuwa nchi yetu inafikia malengo ya kitaifa na kimataifa kama vile malengo endelevu ya Milenia 2030 yanayotutaka kupunguza athari za vifo vitokanavyo na uzazi hadi kufikia vifo chini ya 70 katika kila vizazi 100,000 vifo vya Watoto chini ya 38 katika kila vizazi hai 1,000 pamoja na vya Watoto chini 12 katika vizazi hai 1,000, " amesema Waziri Ummy.

Ameongeza  Serikali imeendelea kuwekeza katika afya ya mama na mtoto kwa kujenga vituo vya huduma za upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni (CEmONC) kutoka vituo 340 mwaka 2021 hadi kufikia vituo 523 mwaka 2023.

Waziri Ummy amesema maboresho ya upatikanaji huduma hizo katika vituo vya kutolea huduma za afya yamesogeza huduma hizo za upasuaji karibu na wananchi. zaidi ya asilimia 75  85 ya wananchi wanapata huduma za Afya ndani ya Kilometa 5 ndani ya maeneo wanayoishi. 

Pia Serikali imeendelea kuwekeza katika Huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto kwa kujenga Wodi za uangalizi maalumu (NCU za watoto wachanga) zinazohudumia watoto wachanga walio mahututi kwa mara mbili zaidi kutoka 99 mwaka 2021 hadi 189 mwaka 2023. 

Amesisitiza hizo  ni hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kutoa huduma bora za afya na kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa wakiwa chini ya kilo moja.

Sambamba na kuboresha huduma hizo Serikali imeendelea kununua na kusambaza vifaa tiba na dawa hivyo kuongeza wigo wa upatikanaji bidhaa za afya ya uzazi kutoka asilimia 82.5 mwaka 2022 hadi kufikia asilimia 88.2 mwaka 2023.

Aidha Serikali imeendelea kuajiri na kupeleka watumishi wenye sifa katika Vituo vya kutolea huduma za afya nchi nzima kuajiri watumishi wa afya wapatao 28,759 hadi kufikia mwaka 2023.

Kwa upande wa Vitanda vya kutolea huduma za afya ya uzazi, amesema  Serikali kwa kushirikiana na wadau imeendelea kuboresha upatikanaji wa vifaatiba hivyo kwa ajili ya huduma za afya ya uzazi huku akifafanua hali ya vitanda vya kutolea huduma kwenye vituo vya afya imeongezeka kutoka vitanda 84,162 (mwaka 2021) hadi vitanda 104,687 (mwaka 2023).

Waziri Ummy amesema anamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ununuzi wa vifaa tiba hivyo ambavyo vina thamani ya Sh.14,953,854,357 ambavyo ni vitanda vya wagonjwa (3080), vitanda vya kujifungilia (1000), magodoro (5500), mashuka (36808), meza za vitanda . Vifaa  hivyo vitasambazwa katika Majimbo yote 214 nchini Tanzania Bara. 

Aidha wanategemea kupokea vifaa tiba vingine hivi karibuni ambavyo ni vitanda vya kujifungulia (4280), vitanda vya kufanyia uchunguzi (examination table) 4280, mkoba wa vifaa vya kujifungulia (delivery kit) 4280, kabati za vitanda (bed side lockers) 6420 na stendi ya dripu (6420).

"Katika kila jimbo tutagawa Kila jimbo litapata Kila jimbo litapata Vitanda 30; Magodoro 30; Mashuka 60; Bed side locker 30; Drip Stand 30; Meza ya kulia chakula 15; Vitanda vya kujifungulia 10; Delivery set 10 pamoja na Examination bed 10. 

"Wabunge watavikuta vifaa hivi kwenye vituo viwili katika kila jimbo ambako MSD watashusha mzigo.Nina imani vifaa hivi vinavyotolewa leo vitachangia katika kuboresha zaidi huduma hizi za mama na mtoto. Nitoe rai kwa Bohari ya dawa kuhakikisha vifaa tiba hivi vinasambazwa kwa wakati."

Aidha  amewashukuru wananchi wote wanaoendelea kutoa taarifa mbalimbali kuhusu changamoto wanazokutana nazo katika kupata huduma za afya vituoni. Sekta ya Afya itaendelea kupata ufumbuzi wa changamoto zinazojitokeza."Tunawaomba muendelee kutoa taarifa kwa kupiga simu ya bure 199 BURE au mitandao yetu ya kijamii ya Wizara."

Pia amemshukuru Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuonyesha dhamira yake ya dhati katika kuboresha zaidi huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto. 

"Sote ni mashahidi wa uwekezaji mkuwa ambao Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameuelekeza katika huduma za afya ya uzazi na sisi tunaahidi kuendelea kumuunga mkono Rais wetu katika kuborsima mi ana kuboresha zaidi huduma za Afya ya Uzazi Mama na Mtoto nchini Tanzania. "











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...