Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe.Abdulaziz M.Abood amekabidhi Gari ya kubebea wagonjwa  (Ambulance)  Hospitali ya Wilaya ya Morogoro Mjini litakalosaidia kupunguza fivo vya mama na mtoto.

 Ambulance hiyo imetolewa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni matokeo ya  maombi ya Mhe. Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini  kwa ajili ya  Hospitali hiyo.

Katika makabidhiano hayo, viongozi  mbalimbali wa chama Serikali walishiriki ikiwemo Mkurugenzi  wa Manispaa  ya Morogoro Ally Machela, wakuu wa Idala ya Afya, Uchumi na Manunuzi.

Akizungumza katika Halfa hiyo Mhe. Abood amempongeza na kumshukuru kwa dhati Mhe. Dkt. Samia kwa gari  la kubebea wagonjwa alioitoa kwa ajili ya Wananchi wa Morogoro Mjini ambao awali walikuwa wanapata changamoto  ya usafiri wakipata rufaa ya kutoka kwenyw vituo vya afya kwenda Hospital  ya Rufaa ya Morogoro.

"Namshukutu sana Mhe. Rais kwani amekuwa msikivu kila ninapomuomba kutatua changamoto  za wana Morogoro Mjini, ametoa fedha nyingi katika ujenzi wa Miradi ya Afya, Ununuzi wa Vifaa na Vifaa tiba vya kisasa na huduma za Dawa kwa ajili ya kutolea huduma katika Jimbo la la Morogoro Mjini." Alisema Abood

Pia Mhe. mbunge amewapongeza Madaktari na wahudumu wote wa afya katika Hospitali ya Wilaya, Divisioni ya Afya na maendeleo ya Jamii sambamba na Viongozi wa Halmashauri wakiongozwa na Mkurugenzi wa manispaa kwa Kazi nzuri wanazozifanya kwenye idara hiyo.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...