Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwa kwenye picha pamoja  na Mkurugenzi wa Kampuni ya China Tourism Group (CTG) ya nchini China, Balozi Dkt. Lu Youqing, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar Es Salaam, Jumamosi Februari 3, 2024, kuhusu masuala mbalimbali. Kulia katika picha ni Ndugu Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Oganaizesheni na kushoto ni Ndugu Rabia Abdalla Hamid, Katibu wa NEC CCM Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Kampuni ya China Tourism Group (CTG) ya nchini China, Balozi Dkt. Lu Youqing, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar Es Salaam. Katika mazungumzo hayo, yaliyofanyika Jumamosi, Februari 3, 2024, viongozi hao wamejadiliana masuala anuai, ikiwa ni pamoja na kudumisha uhusiano na kuimarisha ushirikiano wenye manufaa ya pande zote mbili, Tanzania na China. Wengine katika picha, kutoka kushoto ni Ndugu Rabia Abdalla Hamid, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na anayefuatia ni Ndugu Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa NEC CCM Taifa, Oganaizesheni
 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akikabidhi zawadi ya kitabu kiitwacho "Misingi ya Falsafa, Itikadi na Sera za Chama Cha Mapinduzi" kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya China Tourism Group (CTG) ya nchini China, Balozi Dkt. Lu Youqing, baada ya viongozi hao wawili kumaliza mazungumzo yaliyofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam, Jumamosi, Februari 3, 2024, kuhusu masuala mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...