HAGE Geingob Rais wa Taifa la Namibia amefariki dunia akiwa na miaka 82 kutokana na maradhi ya saratani yaliyokuwa yanamsumbua.

Kwa mujibu wa shirika la Utangazaji la Al-Jazeera imeripotiwa kuwa Hage amefariki dunia leo jumapili katika hospitali ya Lady Pohamba akiwa amezungukwa na mke pamoja na watoto. 

Aidha makamu wa Rais wa Taifa hilo Nangolo Mbumba ametoa taarifa ya kifo hicho kupitia ukurasa rasmi wa mtandao wa kijamii wa Facebook wa Hage Geingob na kuwataka raia wa nchi hiyo kutulia wakati Serikali ikifanya taratibu za mazishi.

Mwezi uliopita Ofisi ya Geingob ilitangaza kuwa kiongozi huyo ameanza matibabu ya saratani ambayo haikuelezwa kwa undani zaidi.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...