Mwandishi Wetu, Babati

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara Anna Mbogo amewahamasisha viongozi wa vikundi 10 vilivyomo katika eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Burunge (WMA), kuhifadhi kumbukumbu zao za fedha kwa usahihi ili kuepusha migogoro itakayosababisha vikundi hivyo kuvunjika.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu Kwa viongozi wa vikundi hivyo, iliyoandaliwa na Taasisi ya Chemchem Association inayofanya shughuli za uhifadhi katika Jumuiya ya Hifadhi Burunge iliyopo mkoani Manyara.

Amesema baadhi ya mambo yanayosababisha vikundi kuvunjika ni pamoja na kutotunza kumbukumbu kwa usahihi na kutumia fedha za kikundi bila utaratibu ambapo amewataka viongozi hao kutokuhifadhi fedha majumbani na badala yake kufungua akauti ya kikundi benki kulingana na sera ya fedha ya jamii ya mwaka 2019.

"Serikali inathamini sana vikundi vya kuweka akiba na kukopa kwani vikundi vinachochea maendeleo ya jamii hivyo viongozi wa vikundi mnapaswa kuwa waaminifu kwa pesa za kikundi ili kujenga imani kwa wanakikundi," alisema Mkurugenzi huyo.

Awali, Meneja Mkuu wa Chemchem Association Clever Zullu, amesema wanajivunia kuwezesha vikundi hivyo kukopesheka na furaha yao ni kuona matunda ya uhifadhi yanaoongozwa na wananchi wenyewe kunufaika.

Amevitaja vikundi 10 vinavyosimamiwa na Chemchem Association kuwa ni Upendo -B, Marewa, Kigogoni, Datoga, Wacheda, Keja, Esinyati, Mdorii, Upendo -A na Mang'oo ambapo viongozi wa vikundi hivyo watapatiwa mafunzo ya siku tatu ili kuendana na Sera ya Community Microfinance ya 2019 ambavyo vitasajiliwa na kutambuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Babati.

Mkurugenzi wa Chemchem Association Fabian Bausch amesema umoja na mshikamano kati ya vikundi vya kuweka na kukopa vimewezesha kuwakwamua kiuchumi wakazi wa vijiji kumi vinavyozunguka Jumuiya ya Hifadhi Burunge.

Amesema wakati wanaanzisha vikundi hivi mwaka 2017 jamii haikuwa na uelewa mkubwa juu ya kuwa na vikundi vya kuweka na kukopa lakini kwa sasa dunia nzima inafahamu shughuli za uhifadhi zinazofanywa na kuwavutia wageni wengi wanaokuja kutali na kuongeza fedha nyingi za kigeni.

Kupitia fedha hizo Chemchem Association inatejesha kwa jamii kwa kusaidia katika sekta za elimu, afya na mazingira




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...