Na  Raisa Said,Tanga

OFISA Elimu Mkoa wa Tanga Newaho Mkisi amesema uandikishaji watoto wanaojiunga na elimu ya awali mkoani hapa imefikia jumla ya watoto 51, 103 ambayo ni sawa na asilimia 65 ya lengo.

Akizungumza mkoani hapa kuhusu uandilishaji watoto kujiunga na elimu ya awali Mkisi amesisitiza idadi hiyo ya walioandikishwa ni asilimia 65 ya lengo lililowekwa na mkoa la uandikishaji kwa mwaka huu.

"Mkoa umeweka lengo la kuandikisha watoto 78,033 kwa ajili ya kujiunga na elimu ya awali ingawa kuna halmashauri ambazo zimefikia asilimia 65 ya unandikishaji hadi hivi sasa na zipo ambazo bado zinasuasua katiia uandikishaji huo."

Ameongeza juhudi zinafanywa kufikia lengo lililowekwa la mkoa la kuandikisha watoto 78,033 kabla ya tarehe ya mwisho wa zonzi hilo, ambayo ni Machi 31, mwaka huu.

Kuhusu uandikishaji kwa darasa la kwanza,Mkisi amesema jumla ya watoto 61,468 wameandikishwa hadi hivi sasa katika Mkoa wa Tanga, idadi ambayo alieleza kuwa ni asilimia 79.9 ya lengo lililowekwa na mkoa.

“Mkoa umelenga kuandikisha watoto wa darasa la kwanza 79,943 hadi kufikia tarehe ya mwisho wa zoezi la uandikishaji,"amesema  Mkisi

Akizungumzia kuhusu mahudhurio ya watoto waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza amesema hadi hivi sasa jumla ya watoto 33,997 wameanza masomo katika shule walizipangiwa kwa muhula wa kwanza.

“Hiyo ni asilimia 69 ya idadi ya watoto ya watoto walioteuliwa kuingia kidato cha kwanza katika shule mbalimbali za sekondari Mkoani Tanga,” amesema Mkisi huku akifafanua jumla ya watoto 48,738 wamechaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule mbalimbali za sekondari mkoani Tanga.

Pamoja na hayo imeelezwa mojawapo ya changamoto inayosababisha wazazi kuacha kuandikisha watoto na kuwapeleka shule ni suala la kukosa fedha kwa ajili kununulia sare za shule.

Hata hivyo, changamoto hiyo  imeondolewa baada ya Serikali kuamuru watoto wote walioandikishwa kupelekwa shule hata kama wakiwa bado hawajapata sare hizo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Korogwe Vijijini, Sadiki Kalaghe amewataka wazazi kuitikia mwito na kutumia fursa iliyotolewa na Serikali  inayoongozwa na Raisi Dk Samia Suluhu Hassan ya kuondoa vikwazo hivyo na kuwaandikisha na kuwapeleka watoto shule.

Akitoa takwimu za uandikishaji wa watoto, Ofisa Elimu wa Halmashauri hiyo, Kassim Mavoa, alisema kuwa hadi kufikia  January 22, mwaka huu jumla ya watoto 7,006 walikuwa wamekwisha andikishwa kuanza darasa la kwanza, ikiwa ni asilimia 91 ya watoto 7,705 ambao walikuwa wanatarajiwa kuandikishwa katika Halmashauri hiyo.

Alisema kuwa alikuwa na matumaini kuwa hadi kufikia mwisho wa mwezi wa tatu ambao ni mwsho wa zoezi hilo la uandikishaji, watakuwa wamefikia asilimia 100. “Mwaka jana tulifikia asilimia 99,” amesema.

Akizungumzia mbinu walizotumia kuhamaishiha uandikishaji, amesema kuwa waliagiza walimu wa wakuu wa shule kuitisha vikao vya wazazi na kutoa matangazo katika maeneo yote kwa ajili ya kuhamasisha uandikishaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...