Na Mwandishi wetu- Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama ameipongeza Serikali kwa kuboresha maslahi ya watumishi nchini kwa lengo la kuinua hali zao za kiuchumi ili waweze kumudu gharama za Maisha na kutekeleza majukumu yako katika mazigira rafiki.

Waziri Jenista ameyasema hayo wakati akizungumza na ujumbe Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Dkt. Jane Madete ambapo alisema ni dhamira ya Rais wa Awamu ya Sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha watumishi maslahi yao yanaboreshwa.

Amesema kuwa kwa kipindi cha muda mfupi Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ametekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule, hospitali, zahanati na kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba katika maeneo mbalimbali nchini.

“Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa kiongozi mahiri ndani ya kipindi kifupi sisi wenyewe ni mashahidi ametekeleza miradi mikubwa sana ya maendeleo na amekuwa mstari wa mbele kuboresha miundo mbinu ya wafanyakazi ili muweze kutoa huduma vizuri na anawapenda sana wafanyakazi,”Alisema Mhe. Jenista.

Pia Waziri Jenista ameupongeza uongozi wa TUGHE kwa kuendelea kuimarisha Chama hicho kikizingatia misingi na katiba ya chama huku akihimiza ushirikiano baina yao hatua itakayosaidia kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku na kuchochea maendeleo ya Taifa.

“Niwapongeze kwa ziara yenu leo, mmeendelea kusimamia katiba ya chama, kujenga ustahimilivu , kuvumiliana na kujenga umoja ili kuimarisha chama kwahiyo kwa niaba ya Seraikali ninawapongeza sana kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kuwaweka watumishi wote pamoja kwa amani,”Alipongeza.

Aidha aliwasisitiza kuendelea kuzingatia sheria na taratibu za utumishi wa umma pamoja na kufanya kazi kwa moyo wa kujitolea na ubinifu kwa manufaa ya Nchi nzima na wananchi kwa ujumla.

“Nitoe wito endeleni kushikimana, kukifanya chama chenu kuheshimika hali itakayovutia kupata wanachama wengi zaidi . Pia mzingatie sheria za Nchi pamoja na kuwasisitiza wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii na kuwa tayari kuelezea mafanikio yenu na kuishauri Serikali maeneo ambayo inaweza kuboresha,”Alieleza.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa TUGHE Dkt. Jane Madete alibanisha kwamba lengo la ziara yao kutambua mchango wake mkubwa katika Chama hicho pamoja na kujadili kwa pamoja namna ya kutatua changamoto zinazowakabili wafanyakazi na kuipongeza Serikali katika uboreshaji wa huduma za wananchi.

“Ujio wetu huu ni kupongeza Serikali kwa namna inavyoboresha huduma kwa wananchi husudani sekta ya afya tumeona hospitali nyingi zimejengwa kuanzia katika vijini hadi mikoa na tumemshauri Mhe. Waziri waone umuhimu wa kuwekeza katika miundombinu ya hospitali zilizojengwa kwa muda mrefu ili kurahisisha utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi,”Alieleza Dkt. Jane.

Aidha Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha wafanyakazi Mhe. Janejelly Ntate aliwasihi wafanyakazi kuendelea kuiamini Serikali ya Awamu ya Sita kwani imeendelea kutikiza ahadi zake kwa vitendo na kuwataka wafanyakazi kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...