Mhe. Balozi Kasike akutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Ufalme wa Eswatini, Mhe. Thulisile Dladla.

Mazungumzo hayo yalifanyika tarehe 28 Machi, 2024 Jijini Mbabane ambapo Mhe. Balozi Kasike alikwenda kumsalimia Mhe. Dladla wakati akiendelea na Ziara yake ya Kikazi nchini Eswatini.

Wakati wa mazungumzo hayo, Mhe. Dladla, aliahidi kwamba Serikali yake itatoa kila aina ya ushirikiano kwa Mhe. Balozi Kasike ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Kwa upande wake, Mhe. Balozi Kasike aliishukuru Serikali ya Ufalme wa Eswatini kwa ushirikiano aliopata wakati wote akiwa nchini Eswatini na kusisitiza umuhimu wa kutekelezwa masuala yote yaliyokubalika wakati wa ziara hiyo kwa maslahi ya Serikali na wananchi wa Tanzania na Eswatini.

Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania - Maputo
30 Machi, 2024Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...