Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani wafanyakazi wa Benki ya NBC  sambamba na wadau wao mbalimbali akiwemo mmoja wa mabalozi wa benki hiyo msanii Jaivah waliungana na mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji wa huduma hiyo muhimu.

Zoezi hilo la uchangiaji damu lilifanyika kwenye viunga vya makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kwa uratibu wa Umoja Wanawake wa benki hiyo ‘NBC Women Network Forum’ ambao pamoja na zoezi hilo pia umoja huo umeratibu hafla fupi zilizohusisha wafanyakazi wa benki hiyo kwenye matawi yake mbalimbali nchini.

Benki hiyo pia ilitumia maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ya ‘Wekeza kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii” kugawa zawadi mbalimbali kwa wateja wake ikiwa ni muendelezo wa kampeni yake ya ‘NBC Buruda Time’ inayopambwa na msaani Jaivah. Mbali na kukabidhi zawadi mbalimbali kwa wateja, msanii huyo pia alipata wasaa wa kuwaburudisha wafanyakazi wa benki hiyo.

Wakizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wenzao Bi Asha Mustafa na Bi Johari Ntambwe ambao pia viongozi waandamizi wa Umoja Wanawake wa benki hiyo walishukuru na kupongeza juhudi zinazofanywa na uongozi wa benki hiyo katika kusaidia wanawake wakiwemo wafanyakazi pamoja wajasiriamali katika kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao. Walisisitiza umuhimu wa kuwekeza katika wanawake na kuhakikisha fursa sawa zinapatikana kwa kila mtu, bila kujali jinsia.

“Kwa ujumla, maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yamekuwa ya mafanikio makubwa na yametupa fursa wafanyakazi wa Benki ya NBC na wadau wetu mbalimbali wakiwemo wateja kushirikiana katika kuchangia jambo muhimu la uchangiaji wa damu. Kupitia ‘NBC Women Network Forum’ tulijipanga kuhakikisha tunayatumia maadhimisho haya kuleta mabadiliko chanya katika jamii na kuendeleza maendeleo ya taifa letu tunashukuru tumefanikiwa.’’  Alisema Bi Ntambwe

Bi Alitoa wito kwa jamii kuzidi kusaidiana na kushirikiana katika kuleta maendeleo ya pamoja. Aliwashukuru wafanyakazi wa benki hiyo kwa kujitolea kuchangia damu na kufanya hafla hiyo kuwa ya mafanikio makubwa.

Katika hafla hiyo, mbali na kupokea zawadi baadhi ya wateja wanawake wa benki hiyo walipata fursa ya kutoa maoni yao kuhusu huduma zinatolewa na benki hiyo ambapo mmoja wa wateja wa hao Bi. Maria Kapinga, alitoa shuhuda ya jinsi benki ya NBC ilivyomsaidia kukuza biashara yake na kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa.

Kwa upande wake msanii Jaivah alitoa wito kwa jamii kuendelea kuchangia damu kwa wingi kwa kuwa inaokoa maisha ya watu ya watu wenye uhitaji. Alisisitiza umuhimu wa kila mtu kuchangia damu mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa mahitaji ya hospitali yanafikiwa na kuokoa maisha ya watu wengi zaidi.

‘’Kupitia kampeni ya 'NBC Buruda Time', tumekuwa tukitoa zawadi na burudani kwa wateja wetu kama sehemu ya kushukuru kwa uaminifu wao. Kupitia maadhimisho tumeweza kutoa zawadi muhimu kuliko zote ambayo ni zawadi ya damu kwa wenzetu wenye uhitaji kwenye hospitali mbalimbali. Tunawahimiza wateja wetu waendelee kufurahia huduma bora za kibenki zinazotolewa na benki hii,’’ alisisitiza Jaivah.

Balozi wa  kampeni ya ‘NBC Buruda Time’ inayoendeshwa na Benki ya NBC msanii Jaivah (Kushoto) akichangia damu sambamba na wafanyakazi wa benki hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Zoezi hilo la uchangiaji damu lilifanyika kwenye viunga vya makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kwa uratibu wa Umoja Wanawake wa benki hiyo ‘NBC Women Network Forum’.Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC wakichangia damu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.


Benki hiyo pia ilitumia maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ya ‘Wekeza kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii” kugawa zawadi mbalimbali kwa wateja wake ikiwa ni muendelezo wa kampeni yake ya ‘NBC Buruda Time’ inayopambwa na msaani Jaivah
Wafanyakazi wa Benki ya NBC Makao makuu wakijipongeza wakati wa hafla fupi ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kwa uratibu wa Umoja Wanawake wa benki hiyo ‘NBC Women Network Forum’. Umoja huo pia uliratibu hafla fupi zilizohusisha wafanyakazi wa benki hiyo kwenye matawi yake mbalimbali nchini.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...