Na Mwandishi Wetu

SHIRIKISHO la Wenye Viwanda nchini (CTI), limekipongeza kiwanda cha nondo na mabati cha Lodhia Industries Ltd kutokana na uwekezaji mkubwa walioufanya na kupelekea ajira nyingi kwa watanzania.

Pongezi hizo zilitolewa na Mkurugenzi wa shirikisho hilo, Leodegar Tenga, wakati ujumbe wa shirikisho hilo ulipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kisemvule Mkoani Pwani na kujionea shughuli za uzalishaji kiwandani hapo.

Tenga amesema bidhaa zinazotengenezwa na kiwanda hicho yakiwemo mabati, nondo na plastiki ni nguzo muhimu katika maendeleo ya nchi kwani ujenzi wa miundombinu unategemea kuwepo kwa bidhaa hizo.

“Unapojenga barabara, madarasa, madaraja na miundombinu yote unahitaji chuma kwa kiasi kikubwa sana sasa sisi tunajisikia fahari sana kuona mwanachama wetu Lodhia amewekeza kwa kiwango kikubwa kama mnavyoona wenyewe,” alisema Tenga

“Lodhia anatekeleza maono ya serikali ya awamu ya sita ambayo siku zote inasisitiza na kuhamasisha uwekezaji kupitia ujenzi wa viwanda vidogo na vikubwa kama hivi vya nondo na plastiki na tunafurahi zaidi kuona mwekezaji huyu ni mtanzania,” alisema Tenga

Aidha, Tenga amewaomba watanzania kuwaunga mkono wazalishaji wa ndani kwa kununua bidhaa zao kwani zina ubora wa kimataifa na wakati mwingine zinazidi viwango vya baadhi ya bidhaa za nje.

“Bidhaa hizi zina ubora wa hali ya juu na nitafurahi kama nitaona watanzania wanachangamkia bidhaa za viwanda vya ndani zikiwemo za nondo, mabati na plastiki kutoka Lodhia ili kuendelea kulinda ajira za watanzania ambao wamepata ajira,” alisema

Aidha Tenga ameiomba serikali na taasisi zake kuendelea kununua bidhaa za viwanda vya ndani zikiwemo ndono na bidhaa za plastiki zinazozalishwa na kiwanda cha Lodhia kama sehemu ya kulinda viwanda vya ndani.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda hicho, Manoj Gopi, ameiomba serikali kuweka mkakati kabambe kulinda viwanda vya ndani kama zinavyofanya baaadhi ya nchi jirani kwa kuhakikisha zinanunua kwa wingi bidhaa kutoka kwenye viwanda hivyo.

Amesema hatua hiyo itasaidia kukuza viwanda hivyo na kuongeza nafasi za ajira kwa watanzania wengi wanaofanya kazi kwenye viwanda hivyo na kulinda hifadhi ya dola ambayo imekuwa ikitumika kuagiza bidhaa nje ya nchi.

Ameongeza kuwa, bidhaa zinazozalishwa na kiwanda hicho zimekidhi vigezo vyote vya kimataifa hivyo haoni sababu yoyote kwa serikali kuendelea kuagiza bidhaa za nje kwaajili ya kutekeleza miradi yake ya miundombinu.

Aidha, amesema wamekuwa wakiuza nondo kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali ya serikali ukiwemo ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi, bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerere Rufiji Mkoa wa Pwani na miradi mingine ya barabara.

“Wenzetu Kenya wameweka sheria kali sana za kulinda viwanda vyao na Uganda wamefanya hivyo hivyo sasa na hapa kwetu kuna umuhimu wa kuendelea kulinda viwanda kwa kuacha kuagiza nje bidhaa kama nondo na bidhaa za plastiki ambazo zinazalishwa hapa nchini na zina viwango vya kimataifa,” amesema

" Lodhia Industries inawekeza dola za Marekani milioni 60 kwenye ujenzi wa kiwanda cha mabati katika eneo hilo ambacho kinatarajiwa kuanza kuzalisha mabati kuanzia mwezi Mei mwaka huu kitakachotoa ajira zaidi ya 500 za moja kwa moja..., kwenye kiwanda cha nondo na bidhaa za plastiki tumewekeza dola za Marekani milioni 45 na kuwezesha ajira zaidi ya 2,000 za moja kwa moja." Amesema

“Uwekezaji huu ni mkubwa sana tunaomba serikali iweke mikakati ya kutulinda na kutupa kipaumbele kwa kununua bidhaa zetu, serikali inapigia debe viwanda kwasababu ndivyo vinakuza uchumi na kuongeza ajira,” alisema

Pia ameiomba taasisi za serikali kama Shirika la Viwango nchini TBS na Tume ya Ushindani FCC kufanyakazi kwa karibu na viwanda hicho kuhakikisha kunakuwa na biashara ya ushindani dhidi ya bidhaa kutoka nje ya nchi.

“Lodhia inaviwanda 15 hapa nchini sasa unaweza kuangalia tumeajiri watanzania wangapi kwa hiyo kukua kwa viwanda vyetu ni afya kwa uchumi wa nchi na kadiri tunavyokuwa ndivyo tunazidi kuongeza ajira kwa watanzania wenzetu,” alisema
 

Mkurugenzi wa Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI), Leodegar Tenga akizungumza na viongozi wa kiwanda cha kuzalisha nondo na bidhaa za plastiki kama mabomba cha Lodhia Industries cha kisemvule Mkuranga mkoa wa Pwani walipotembelea kiwanda hicho

 

Viongozi wa CTI na Lodhia Industries wakianza ziara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...