Raisa Said,Tanga

Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji Tanga, Dk Frederick Sagamiko kuwasimamisha kazi watumishi watano kutoka katika kituo cha afya cha Mikanjuni kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mama mmoja ambaye alijifungua kwa njia ya upasuaji.

Watumushi hao wanaotuhumiwa kwa uzembe ulisaobaisha mama huyo, Fatma Musa Selemani kuwekewa damu kinyume na utaratibu kitu ambacho kilisababisha kupata mzio na hatimaye kufa.

Alisema kuwa serikali imeamua watumishi hao ambao ni madaktari wawili na wauguzi watatu wasimame kazi hadi hapo tume husika itakapo kamilisha uchunguzi na kubaini makosa yao.

“Taarifa za awali zinasema kuwa kulikuwa na mgonjwa ambaye alikuwa anahitaji kuwekewa damu katika wodi ambayo pia alilazwa mama huyo mkazi wa Magaoni ambaye alijifungua mtoto kwa njia ya upasuaji,” alisema Kaji

Aliendelea kuelezwa kuwa kwa kuwa hakukuwepo na umakini wa kuachiana taarifa sahihi uzembe huo ulisababisha muuguzi aliyekuwepo zamu kumuwekea damu mama huyo, jambo ambalo lilisababisha yeye kupata mzio na hatimaye kufariki dunia.

Kaji aliwataja watumishi ambao kuwa ni muuguzi aliyekuwa zamu mchana, Fadhili Ali Hoza, wauuguzi wengine waliokuwepo usiku Restituta Kisendo Deusdedit na Muya Ali Mohamed. Aliwataka madaktari kuwa ni Dk Andrew Eliyasikia Kidee, na k Hamis Mohamed Msanii.

Kwa mujibu wa maelezo mama huyo alilazwa katika kituo hicho tarehe 27 mwezi huu akiwa na uchungu, saa tisa mchana na ambapo alielezwa kupata uchungu pingamizi na hivyo madaktari kulazimika kumzalisha kwa njia ya upasuaji,

Mkuu huyo wa Wilaya alitoa pole kwa wafiwa na kueleza masikitiko yake na ya serikali juu ya kifo hicho na kusema serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan haitavumulia uzembe kama huo ambao alisema umeonekana kuaza kushamiri katiika sehemu mbambali nchini hivi sasa katika vituo mbalimbali.

Aliwaonya watumishi wa afya na kuwataka kuwa makini katika kazi ili kuzuia matukiio kama hayo yayasababishwa na uzembe.

Dada wa mama huyo alijitambulisha kwa jina la Dhamna Bakari Mzia alisema kuwa yeye mwenyewe marehemu aliwapigia simu kuwataarifu kuwa amejifungua kwa njia ya upasuaji, hivyo wakaondoka kwenda katika kituo hicho akiwa ameongozana na mume wa huyo marehemeu.

“Tulipofika nikaonyeshwa mtoto, nikaambiwa mama mtoto huyu hapa. Halafu nikaenda kwa mgonjwa nikaangalia mtoto na mgonjwa. Baada ya hapo Daktari akaniambia mgonjwa hana damu, anahitaji kuwekewa damu. Mimi nikamwambia kuwa mimi sijui lakini daktari akikuambia kitu unaridhika nacho,” alisema Mzia.

Aliendelea kueleza kuwa muda ulipofika akawekewa damu ambapo mwanzo ilikuwa inaleta tabu lakini baadaye ikaenda vizuri. Baada ya hapo mgonjwa akasema anaomba chai na akamuliza daktari kama muda wa kunywa chai mgonjwa umefika?

“Nikamwekea nusu kikombe nikamuuliza utaweza kunywa akasema staweza lakini nataka chai ikabidi nimnyanyue nikamnywesha nusu ya kwanza, akaniambia niongeze chai nikamuuliza tena daktari nimowngeze akasema ndio. Nikamwongeza lakini baada ya hapo hali ikaanza kuwa mbaya,” alisema Mzia.

Alieleza kuwa madaktari walipofika akaambiwa aondoke ili mgnjwa ahudumiwe. B zia lisema kuwa aliondoka kama alivyoambiwa alipooelezwa kuwa mgonjwaa mefariki.

Hata hivo Mume wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Rashid Juma ameomba watu kama hao wanaokuwa wazembe na kusababisha matukio kama hayo wachukuliwe hatua kali kwa sababu bila hivyo uzembe huo utaendelea .



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...