Na Janeth Raphael - MichuTv - Dodoma

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt Samia Suluhu Hassan amejitoa kuwa Kinara kwa kuibeba ajenda ya Matumizi ya Nishati safi Barani Africa.

Raisi Samia amesema hayo wakati alipozungumza kwa njia simu na wadau mbalimbali wakiwemo wanawake kutoka maeneo tofauti hapa Nchini katika Kongamano la wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya Nishati safi ya kupikia 2024 lililofanyika mapema leo hii Jijini Dodoma.

Na kuongeza kuwa ahadi yake ni kuibeba Nchi yetu kadri atakavyoweza katika suala hili.

"Mimi kiongozi wenu naibeba ajenda ya Nishati safi ya kupikia,ndani ya Bara la Africa Mimi ndio Champion wao".

"Lakini pia ahadi yangu kwa Wizara ya Mazingira kwako Makamu wa Raisi na Nishati pia,nitaibeba hiyo ajenda nikisaidiwa na ninyi,ni kwamba nitaibeba Nchi yetu kadili nitakavyoweza kwenye suala hili".

Katika Hotuba yake Mgeni Rasmi Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt Philip Mpango amesema kuwa hapa Tanzania Takribani hekta 469,420 za misitu hupotea kila mwaka kwa Shughuli za kibinadamu ikiwemo ukataji wa miti kwaajili ya kuni na mkaa Hali inayopelekea uharibifu na hata kwenye vyanzo vya maji.

"Hapa Tanzania Takribani asilimia 90 ya kaya hutumia kuni na mkaa kama nyenzo kuu ya Nishati ambapo asilimia 65 ya Nishati inayotumika majumbani ni kuni, asilimia 26.2 ni mkaa na asilimia 8.8 ni mjumuisho wa gesi,umeme na vyanzo vingine".

"Kutokana na Matumizi Takribani hekta 469,420 za misitu hupotea kila mwaka kwa Shughuli za kibinadamu ikiwemo ukataji wa miti kwaajili ya kuni na mkaa,Hali hii huchangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira kupelekea hata kukauka kwa vyanzo vya maji".

Aidha Makamu wa Raisi ameeleza kuwa wanawake ndio waathirika wakubwa wa matumizi ya Nishati chafu,kukutana changamoto katika utafutaji wa kuni ikiwemo vitendo vya ukatili wa kijinsia.

"Waheshimiwa viongozi na wadau wa Kongamano hili, wanawake ndio waathirika wakubwa wa matumizi ya Nishati chafu ya kupikia, inakadiliwa kuwa katika maeneo mengi ya vijijini wanawake wanatumia masaa 20 kwa wiki kutafuta kuni na hivyo kushindwa kujihusisha na Shughuli za Maendeleo lakini pia kuna changamoto nyingi wanazokutana nazo katika utafutaji wa kuni ikiwemo kukutana na nyoka na hata kukumbwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia".

Naye Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Ditto Biteko ametumia nafasi hii kuwaomba Wakuu wa Mikoa,Viongozi wa dini,Wababa katika familia zao na vyombo vya habari kutumia muda wanaoupata kuelezea umuhimu wa matumizi ya Nishati safi kwa watu wanaowazunguka.

"Hebu tuibebe hii ajenda kwa pamoja Wakuu wa Mikoa, Viongozi wa dini katika mahubiri yenu tafuteni sentensi mbili tatu kuwaambia waumini wenu umuhimu wa matumizi ya Nishati safi,wakina Baba nyumbani wakati mnazungumza na watoto wapeni sentensi mbili tatu wakue wakijua umuhimu wa matumizi ya Nishati safi".

Kongamano hili limehudhuliwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, Wadau wa Nishati na wanawake kutoka sehemu mbalimbali hapa Nchini.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Wadau mbalimbali walioshiriki kongamano la Nishati Safi ya Kupikia lililofanyika leo katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma. Kongamano linalokwenda pamoja na ugawaji wa mitaji na vitendea kazi vya Nishati Safi ya Kupikia. NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto BITEKO akizumza na wadau mbalimbali katika Kongamano hilo

Wadau mbalimbali  wakiwa kwenye Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia lililofanyika  leo katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...