Katibu wa NEC Idara ya Organaizesheni na Mlezi wa Jumuiya zote za Chama Cha Mapinduzi Ndg. Issa Gavu amefunga Mafunzo Maalum kwa Viongozi wanawake Kutoka mikoa 9 ya Kanda ya ziwa na kanda ya ziwa Magharibi.

Comred Issa Gavu amefunga mafunzo hayo yaliyohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Chama na Jumuiya ya wanawake Tanzania wakiongozwa na Mwenyekiti wa UWT Ndg. Mary Chatanda yaliyofanyika Mkoani Mwanza .

Lengo la Mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wanawake namna ya kuchochea Maendeleo ya Nchi na kuleta ufanisi wa Utendaji kazi katika Jamii na kujikwamua Kiuchumi.

Comred Issa Gavu amewasihi Viongozi wanawake waendelee kuunga Mkono Juhudi za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, yeye ndiyo Mfano mzuri wa wanawake wote wanao onyesha kwa vitendo kujikwamua kiuchumi na ufanisi mzuri wa kazi, na yeye ndiye anawawakilisha katika ngazi ya Juu ya Uongozi wa Nchi.

Mafunzo hayo yaliyofungwa Mkoani mwanza katika Ukumbi wa Winterfell yamehusisha viongozi kutoka Mikoa ya Mwanza, Kagera, Katavi,Shinyanga, Simiyu,Geita, Kogoma,Tabora na Mkoa wa Mara leo Tarehe 27 Machi 2024.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...