Katika kusherekea siku ya wanawake Duniani  kampeni ya Strategis Insurance yenye makao yake mkuu Masaki jijini Dar es salaam imepeleka misaada mbalimbali katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam ili kusaidia  wagonjwa kina mama na watoto wanaopatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

Akiongea wakati wa hafla hiyo, Afisa Masoko wa kampuni hiyo, Bi. Fatma Kilinda (pichani juu) , amewaambia wanahabari kwamba kampuni ya Strategis inasisitiza sana umuhimu wa kila Mtanzania  kuwa na Bima ya Afya.


 "Nchi yetu karibuni itaingia katika mfumo wa Bima ya Afya kwa kila mtu. Hivyo basi, sheria hii itakapokuja kuanza kutumika rasmi sisi Strategis tukiwa moja ya wadau wakuu wa kutoa huduma hiyo tumejipanga vyema katika kuimarisha na kutoa huduma bora.


"Vile vile  tutaendelea pia kutoa elimu kuhusiana na umuhimu wa kila mtu kuwa na bima ya Afya…” amesema Bi Fatma.


Wafanyakazi wa Strategis Insurance wakiwa katika hatua mbalimbali zainazoonesha walipofika katika hospitali ya Mwananyamala, Kinondoni,  jijini Dar es salaam  kutoa misaada  kwa ajili ya kina mama na watoto wanaopatiwa matibabu katika hospitali hiyo ya Rufaa.

Wakiwa na nyuso za tabasamu, wafanyakazi wa Strategis Insurance wakiwa katika picha ya pamoja walipofika katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam  kutoa misaada  kwa ajili ya kina mama na watoto wanaopatiwa matibabu katika hospitali hiyo ya Rufaa,

Katika kusherehekea siku ya Wanawake Duniani wafanyakazi wa Kampuni ya Strategis Insurance wakifurahia na kujipongeza baada ya kutoka hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam kutoa misaada mbalimbali kwa ajili ya kina mama na watoto wanaopatiwa matibabu hospitalini hapo.
Mkurugenzi Mkuu wa kampung ya strategis Insurance,  Dr Flora Minja, akikata cake ya kusherehekea siku ya wanawake duniani katika makao makuu ya ofisi za Strategis iliopo Masaki jijini Dar es salaam. Pembeni yake ni Mkuu wa kitengo cha Utawala Ms Joyse Misson

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...