Mnamo Septemba 1,  1990 Baba Mtakatifu Yohane Paulo II alitua ardhi ya Tanzania katika Uwanja wa Ndege Kimataifa wa Julius K.Nyerere na kubusu ardhi yake.

 

Kwa siku 5 alizuru Dar e salaam,Songea,Mwanza,Tabora na Moshi, abako alikutana  na waamini wa Mungu na wenye mapenzi mema ili kuwaimarisha Imani yao na faraja.

 

Baba Mtakatifu Yohane Paulo II alipotembea Nchini Tanzania, miaka 33 iliyopita kuanzia tarehe Mosi Septemba hadi tarehe 5  Septemba 1990, akiwa  katika ziara yake ya siku 10 ya Bara la Afrika. Pamoja na Tanzania, alitembelea pia Burundi, Rwanda na Ivory Cost kuanzia 1-10 Septemba 1990. Hapa Tanzania alitembelea Dar es Salam, Mwanza, Tabora na Moshi.

 

Katika ziara hiyo ya kitume akiwa katika miji hiyo tajwa Mtakatifu Yohane Paulo II alifanya matukio mbali mbali ambayo ni kuanzia na lile mara alipotua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere

 

Alipowasili alibusu ardhi na alitoa hotuba kwa viongozi wa Serikali, wa kiraia na waliofika kumpokea na wakati huo huo alifanya Mkutano na waamini waliokusanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, jijini Dar es Salaamu, Mkutano wa wanadiplomasia katika Ikulu, Dar Esaalma, na kuhitimisha na Mkutano na Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania (TEC) katika Ubalozi wa Vatican, Oyster Bay mjini, Dare Es Salaam.

 

Tarehe 2 Septemba 1990, alifanya Mkutano na Madhehebu mbambali na kidini katika Uwanja wa Jangwani, Dar Es Salaam;  Mkutano na Makleri na watawa katika Parokia ya Mtakatifu Petro Dar es, Salaam. 

 

Akiwa Songea tarehe 3 Septemba 1990 alitoa kipaimara kwa vijana 100 katika uwanja wa Ruhiwiko Jimbo Kuu katoliki Tanzania. 

 

Mwanza: Alizungumza na Wagonjwa katika Kanisa Kuu la Mwanza tarehe 3 Septemba 1990; Aliadhimisha misa Takatifu katika uwanja mkubwa wa Kawekamo tarehe 4 Setemba 1990. 

 

Tabora: Mtakatifu Yohane Paulo II alitembelea Tabora na katika adhimisho la Neno kwenye Uwanja wa Hassani mwinyi alitoa hotuba yake tarehe 4 Septemba 1990. 

 

Moshi: Tarehe 4 Septemba 2023 Mtakatifu Yohane Paulo II alihotubia waamini waliokuwa katika Kanisa la Kristo Mfalme huko Moshi. Tarehe 5 Septemba 1990 aliadhimisha Misa Takatifu na kuhubiri  katika Uwanja wa Kilimanjaro huko Moshi Tanzania. 

 

Hatimaye  siku ya mwisho katika hafla ya kuagwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro, Tanzania tarehe 5 Septemba 1990.













 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...