Na Mwandishi wetu, Mbulu

MBUNGE wa viti maalum Mkoani Manyara (CCM) Regina Ndege amewasihi madiwanin na wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, kusimamia ipasavyo miradi ya maendeleo ili iwe na tija.

Mbunge Regina ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, kilichofanyika makao makuu yake Dongobesh.

Amesema madiwani na wataalamu wakisimamia ipasavyo fedha za miradi ya maendeleo, ubora wake utakuwa na manufaa kwa jamii husika.

“Ubora wa miradi unaweza kuwa na tija kwa muda mrefu kwa jamii, pindi ikisimamiwa ipasavyo na madiwani pamoja na wataalamu wetu,” amesema Mbunge Regina.

Amesema viongozi hao wakishirikiana kwa pamoja kwa kusimamia vyema miradi ya maendeleo, thamani ya miradi itaonekana na itawanufaisha wananchi wa Mbulu.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Joseph Guulo Mandoo amesema ushauri huo uliotolewa na Mbunge wa viti maalum ni mzuri kwani miradi itakuwa na manufaa kwa jamii.

Mandoo amesema madiwani wa Halmashauri yake na wataalam wao wamesimama kidete kwa kushirikiana na kusimamia miradi yao ya maendeleo ipasavyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...