NA WILLIUM PAUL, MWANGA.

MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ameitaka Wizara ya Maji kuhakikisha mradi wa maji Same – Mwanga – Korogwe unakamilika ifikapo Juni mwaka huu huku akitangaza kujiuzulu nafasi yake endapo mradi huo utashindwa kukamilika.

Dkt. Mpango ametoa kauli hiyo leo alipotembelea chanzo cha mradi huo Nyumba ya Mungu wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro ambapo alisema kuwa, mradi huo umekuwa kero kubwa kwani ulianza tangu miaka 19 iliyopita lakini mpaka sasa haujakamilika.

“Kila mmoja anayehusika katika mradi huu atimize wajibu wake, na mimi nitarudi tena hapa kuangalia huu mradi nikikuta maji hayatoki nitaacha kazi sasa na mimi nikiacha kazi hao wengine sijui Katibu Mkuu Wizara ya maji nja Waziri wako mimi sijui kwa hiyo tuelewane vizuri” alisema Dkt. Mpango.

Alisema kuwa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaimani kubwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya maji ambapo siku ya kumuapisha kwake moja ya mzigo mkubwa aliombebesha ni mradi wa maji Same – Mwanga – Korogwe.

Makamu wa Rais alisema kuwa, Amiri Jeshi Mkuu alitoa amri ya kuhakikisha ifikapo Juni mwaka huu maji yawe yanatoka Same na Mwanga na kuwataka kujipanga vizuri na kuwasimamia Wakandarasi kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha maji yanatokla,

Alisema kuwa, mradi huo umekuwa kero kwa Wananchi wa maeneo hayo ambapo ni takribani miaka 19 tangu kuanza kwa mradi huo ambapo wananchi wameusubiria kwa muda mrefu sasa imefika wakati wananchi wapatiwe maji.

“Kama kunakituo ambacho nitapenda muwe mnakuja mara nyingi mpangiane zamu usiku na mchana Waziri wa Maji na wasaidizi wako ni hapa kwenye huu mradi Amirijeshi Mkuu akishatoa amri ni lazima itekelezwe na maji yatoke” alisema Dkt. Mpango.

Aliwataka pale wanapohisi kunachangamoto wajipange kuyatatua kwani Serikali haiwezi tena kurudi kuwatizama wananchi wa Same na Mwanga na kuwaambia wasubiri tena kidogo.

Aidha Dkt.Mpango alisema kuwa maji ni rasilimali kubwa na ya Taifa kwani bila maji hakuna uhai na kumtaka Mkuu wa Mkoa kuanzia kwenye chanzo cha maji kulinda mazingira na kuyasimamia kwa kushirikiana na Wakuu wa wilaya.
Akisoma taarifa ya mradi kwa Makamu wa Rais, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mwajuma Waziri alisema kuwa, mradi huo ujenzi wake ulianza mwaka 2014 ukiwa na Wakandarasi watatu.

Alisema kuwa, chanzo cha mradi huo kinauwezo wa kuzalisha maji lita milioni 103 ambapo mpaka sasa mradi umeshakamilika kwa asilimia 85.7 na kudai kuwa mradi ukifikia asilimia 92 utaanza kutoa maji na kuhikikisha ifikapo Juni mwaka huu maji yataanza kutoka.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...