Raisa Said,Pangani

Utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Taifa wa Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya Awali (PJT-MMMAM) uliotambulishwa katika Halmashauri ya Pangani hivi karibuni umeleta matumaini mapya ya kuondoa tatizo la ukatili dhidi ya watoto hususani wale wenye umri kuanzia mwaka 0-8 tatizo ambalo linatajwa kuongezeka siku baada ya siku wilayani humo.

Kwa mujibu wa Takwimu za Taifa za Makadirio ya Idadi ya Watu zilizotolewa na Idara ya Taifa ya Takwimu, Tanzania ina takriban watoto 16,524,201 (wakiume 8,328,142 na wakike 8,196,056) wenye umri wa miaka 0-8 (ambayo ni asilimia 30 ya watu wote). Hii ina maana kwamba katika kila watu watatu, kuna mtoto mmoja kati ya umri wa 0 na 8.

Matukio ua ukatili dhidi ya watoto walio chini ya miaka 0-8 yamekuwa yakiripotia maeneo mengi nchini ikiwemo Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga ambapo kwa mujibu wa aliyekuwa mkuu wa Wilaya hiyo ambaywe kwa sasa amehamishiwa Wilaa yab Muheza Bi Zainabu Abdalah matukio ya ukatili dhidi watoto wenye umri wa miaka 0-8 yamekuwa yanajitokeza na kuathiri ukuaji wa wototo kiakili,kisaikolojia na hata kimaumbile.

Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana kutoka kwenye tasnifu ya Uzamili ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ya mwaka 2021 iliyofanywa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zainab Abdallsh ISSA, wilaya hiyo ni moja ya maeneo ambayo yamekumbwa na matukio ya ukatili huu.

Viongozi na wakazi wote kwa pamoja wanatoa wito wa kuimarishwa kwa juhudi za kutokomeza ukatili huo kwa mujibu wa sheria na sera mbalimbali zinazohusiana na malezi na makuzi ya mtoto ikiwemo Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009, Sera ya Maendeleo ya Mtoto (2008) Sera ya Elimu na Mafunzo (2014) na Sera ya Afya (2017) ambayo inalenga kushughulikia mahitaji jumuishi ya maendeleo ya watoto wenye umri wa miaka 0-8.


Kwa mujibu wa Ofisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya hiyo, Kirigiti Matera, kwa sasa kiwango cha ukatili kimefikia asilimia 86 ambapo katika mwezi wa Desemba, mwaka 2023 kulikuwa na kesi tano ambazo zilifikishwa mahakamani. Kesi zote zinahusu ukatili dhidi ya watoto.

"Hali ni mbaya sana. Juzi tu, nilikuwa kortini katika kesi ya ukatili dhidi ya mtoto," alisema Kirigiti wakati Wa mahojiano.

Ofisa Rasilimali Watu wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Veronica Marwa, anakubali kuwa kitakwimu Wilaya ya Pangani inaonekana kuwa na changamoto kubwa ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto wenye umri wa miaka 0-8.

Wataalam,wanaharakati wa haki za mtoto na watafiti wanasema kundi hili la watoto wadogo linatakiwa kuangaliwa kwa kina na kuwekezwa ili waweze kuwa rasilimali nzuri na yenye tija kwa familia na taifa.Uwekezaji unaopaswa kufanywa ni pamoja na kukabiliana na tatizo la udumavu, kuwapatia huduma bora za elimu ya awali na programu za elimu zitakazowawezesha kukua na kufikia ukuaji kamili na hatimaye kuwa watu wazima wenye uwezo wa kuzalisha mali kwa tija na hivyo kuchangia ukuaji wa uchumi. uchumi wa Tanzania pamoja na kujenga jamii yenye amani na utulivu.

Changamoto kubwa zilizobainishwa katika uchambuzi ni udhaifu wa mfumo wa uratibu na utoaji wa huduma shirikishi za malezi kwa watoto wenye umri wa miaka 0-8, zenye ubora na utoshelevu, katika maeneo yote nchini.

Mpango Jumuishi wa Taifa wa Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto unaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2021/22 hadi 2025/26, unalenga kuongeza kasi ya upatikanaji wa matokeo chanya katika makuzi ya mtoto kwa kuboresha mfumo shirikishi wa kisekta. katika elimu ikijumuisha watoto.

Programu hiyo ya MMMAM inaunga mkono utekelezaji wa mifumo ya uratibu kwa kuleta Mpango huu ambao unawaleta Wadau wote kutoka Sekta mbalimbali, Wadau wa Maendeleo na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, asasi za kiraia kushirikiana ili kuhakikisha Watoto (0-8) nchini Tanzania wanapata elimu jumuishi, ustawi na kufikia Ukuaji timilifu.

Mpango huu unatambua uwepo wa programu nyingine za kitaifa zinazotumia mfumo wa kisekta katika maendeleo ya mtoto, ikiwa ni pamoja na Mpango Jumuishi wa Taifa wa Lishe (NMNAP - 2016/2021) na Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA 2017/18 - 2021/22).

Mpango Jumuishi wa Kitaifa wa MMMAM utachangia katika programu zilizopo za kitaifa kwa kuimarisha fursa zilizoainishwa na kukabiliana na mapungufu yaliyopo ili kuboresha utoaji wa huduma shirikishi za matunzo, makuzi na maendeleo ya awali kwa watoto wote (umri wa miaka 0-8) nchini.

Kuanzishwa kwa mpango huo wilayani Pangani mkoani Tanga kutasaidia katika malezi ya watoto kutokana na hali ya ukatili dhidi ya watoto kutajwa kusababishwa na a na ukosefu wa matunzo, malezi na makuzi ya awali ya watoto.

“Mtoto anakulia katika mazingira ambayo anasikia watu wanatukana, anaona ni jambo la kawaida, utekelezaji wa mpango huu utasaidia kuondoa tatizo la ukatili wa kijinsia, kwa watoto wa miaka 0-8” alisisitiza. Marwa.

Alibainisha kuwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani imeandaa programu inayoshughulikia ukatili wa UWAKI. Aliahidi kushirikiana na ofisi hiyo kuona namna ya kuzuia au kutokomeza kabisa ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto wilayani humo,

Anasema pia amewaagiza viongozi wote kuhakikisha wanaingiza masuala ya malezi na makuzi ya mtoto katika bajeti zao kwa kudhani kuwa sasa ni wakati wa kuandaa bajeti.

“Programu hii inahitaji fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wake, lakini hakuna mahali inapoonyesha kuna mdau ambaye ataleta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huo, tunatakiwa kutumia rasilimali zilizopo katika utekelezaji,” alisema.

Bi Marwa anabainisha kuwa amemuagiza Afisa Ustawi wa Jamii wa halmashauri hiyo kufanya uchambuzi wa shughuli za muda mfupi ambazo wanaweza kuanza nazo.

Mkurugenzi wa Shirika lisiro la kiserikali linalojihusisha na masuala ya watoto lenye makazi yake Jijini Tanga ( UHTC) Dk Regis Temba amesema mpaka sasa uzinduzi wa mpango huo umefanyika katika halmashauri zote 11 za mkoa wa Tanga.

Hata hivyo alisisitiza kuwa elimu bado inatakiwa kufika katika ngazi ya kata na vijiji ambapo amesema watu wapo wengi. Pia alizungumzia haja ya kutoa elimu katika kliniki za uzazi ili akina mama wapate uelewa wa kutosha.

Dk.Temba amesema kwa kushirikiana na serikali ya Mkoa na mwandishi kinara wa habari za watoto wataendelea kutoa elimu kwa jamii kupitia vyombo vya habari vya redio,magazeti,mitandao ya kijamii na televisheni ili kusaidia jamii kulea watoto kwa kuzingatia nguzo tano za malezi ya mtoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...