Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Afya ya Mimea na viuatilifu (TPHPA) kanda ya mashariki, imegawa miche ya matunda katika shule ya sekondari za Diplomasia, Uhamiaji, Mwalimu Nyerere na shule Kiungani zilizopo Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Profesa Joseph Ndunguru, Meneja wa kanda ya Mashariki Dk.Mahamudu Sasamalo amesema wamegawa jumla ya miche 60 ikiwa ni juhudi za kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kutaka Watanzania watunze mazingira kwa kupanda miti.

" TPHPA tumeamua kutoa miti ya matunda na hasa mashuleni kwa kuhakikisha kuwa watoto wetu wanapata hewa safi, kivuli na zaidi wapate matunda," amesema.

Ameongeza kwamba TPHPA inaendelea na jitihada za kutunza mazingira kwa vile afya ya binadamu na wanyama ni miongoni mwa jukumu lao huku akisisitiza sote tuna wajibu wa kutunza mazingira na kupanda miti kwani ina faidi nyingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...