Njombe


Ili kupunguza wimbi la watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kushindwa kuhudhuria masomo kutokana na kukosa sare za shule pamoja na mahitaji mengine,Jumuiya ya Umoja wa Wanawake mkoani Njombe imeweza kununua na kugawa sare,sabuni pamoja na madaftari kwa baadhi ya wanafunzi ili kupunguza changamoto wanazokutana nazo.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Scolastika Kevela kwa kushirikiana na UWT wilaya ya Wanging'ombe wametoa msaada huo kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Uhenga ikiwa ni katika kuelekea kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambapo kiwilaya Jumuiya imeadhimisha katika kata ya Uhenga iliyopo wilayani humo.

"Sisi UWT ni walezi na ni wazazi kwa hiyo tumeamua kuwanunulia sare ili waweze kusoma na wasijiskie tofauti na wenzao na hili kumuunga mkono Dkt.Samia katika sekta ya elimu"amesema Scolastika Kevela
Vile vile ameagiza vijana wenye uwezo kulea wazee vijijini kuliko kuwaacha wakihangaka peke yao kwa kuwa ndio wenye bara zao.

"Niache agizo kwa wanawaake tulio na nguvu wote kuwa tuna wajibu wa kuwahudumia wazee,ukiweza nenda kamchotee maji au kampikie ukitaka zaidi kamuokotee kuni yeye atakubariki na sisi hapa leo tumewaletea kanga hizi na sabuni"aliongeza Mama Kevela

Kwa upande wao wanafunzi waliopokea msaada wametoa shukrani zao kwa akina mama kwa msaada huo huku wakiahidi kwenda kusoma kwa bidii zaidi ili kuja kusaidia wazazi wao kwa kuwa sasa wamepunguziwa changamoto.

Hata hivo wanawake wa kata ya Uhenga wameishukuru serikali kwa kuendelea kuwashika mkono kwa kuwa vikundi saba ndani ya kata hiyo vimefanikiwa kupata mikopo inayowainua kiuchumi huku kikundi kimoja kikipata mradi wa ufugaji wa kuku 700 kutoka shirika la kuhifadhi mazingira na kurejesha uoto wa asili.

Nao baadhi ya madiwani wa viti maalumu waliyohudhuria katika hafla hiyo wametoa wito kwa wanawake wa Uhenga kuendelea kufuata utaratibu wa maandalizi ya vyakula bora ili kuondokana na tatizo la udumavu linaloikabili wilaya hiyo na mkoa wa Njombe kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...