Na Mwandishi Wetu, Tanga

UBALOZI Uswisi nchini kwa kushirikiana na Shirika la Amend Tanzania wanaendesha wanaendesha mafunzo ya usalama barabara ikiwemo huduma ya kwanza kwa madereva wa bodaboda zaidi ya 500 katika mkoa wa Tanga

Akizungumza leo Machi 6, mwaka 2024 baada ya kutoa mafunzo kwa madereva wa bodaboda wa Kata ya Magaoni na Mabawa Ofisa Miradi wa Amend Ramadhani Nyaza amesema mafunzo hayo ya usalama barabarani yanatolewa kupitia ufadhili wa Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania na lengo ni kuliwezesha kundi la bodaboda kuepukana na ajali wanapokuwa barabarani.

Aidha amesema kuwa mradi huo kwa ujumla wake umelenga kuwafikia zaidi ya madereva wa bodaboda 750 waliopo katika mikoa ya Tanga na Dodoma.

Amefafanua kwamba katika Mkoa wa Dodoma walishatoa mafunzo hayo na kuwafikia madereva 250 huku akieleza na kwa Mkoa wa Tanga wanatarajiwa kuwafikia 500.

Ameongeza kulingana na takwimu za ajali kuonesha kundi la bodaboda ndio lipo hatarini Amend na Ubalozi wa Uswisi wameona ni wakati sahihi kuendelea mafunzo hayo Ili kupunguza ajali za barabarani.

"Mmradi huo kwa ujumla wake umelenga kuwafikia zaidi ya madereva wa bodaboda 750 waliopo katika mikoa ya Tanga na Dodoma,"amesema na kusisitiza mradi wa kutoa mafunzo hayo kwa bodaboda umekuwa na tija kwani waliopata mafunzo wameendelea kuwa mabalozi wazuri kwa wengine.

Kwa upande wao baadhi ya madereva ambao wamepata mafunzo hayo wamesema yamewasaidia kujua umuhimu wa matumizi ya alama za barabara .

Mmoja wa bodaboda hao Rehema Rashid alisema kuwa mafunzo yameweza kuwa mkombozi katika shughuli zake za kusafirisha abiria kwani awali hakuna na ufahamu wowote ule.

"Nilikuwa naendesha pikipiki lakini sijui lolote lakini baada ya mafunzo haya naelewa hata nikiwa barabara najua kitu cha kufanya Ili kuzuia ajali na kuhakikisha nakuwa salama muda wote"alisema Rashid

Awali Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Mikanjuni Rehema Saidi amewataka vijana kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya usalama wa barabara na jinsi ya kuendesha chombo cha moto kwa usalama na kuepuka ajali.

"Elimu hii ninzuri sana hasa kwa vijana wetu ambao wanaofanya shughuli ya usafirishaji kwa kutumia usafiri wa bodaboda kwani ni mafunzo yanayotolewa bure lakini yatawasaidia uwaepusha na ajali ambazo zinaepukika."





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...