Na Oscar Assenga,TANGA.

WAZIRI wa Michezo,Sanaa na Utamaduni Dkt Damas Ndumbaro amepongeza Mashindano ya Oddo Ummy Cup huku akieleza kwamba watayatumia kuangalia vipaji vya wachezaji na baadae aone namna ya kumpigia simu Kocha wa timu ya Taifa ili kuona namna ya kuwapeleka kwenye Taifa ya Taifa.

Dkt Ndumbaro aliyasema hayo Machi 10 mwaka huu Jijini Tanga ambapo alikuwa mgeni rasmi katika Fainali ya Mashindano ya Mpira wa Miguu ya Oddo Ummy Cup ambayo yameandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kwa lengo la kuibua vipaji vya wachezaji wachanga.

Mashindano hayo hufanyika kila mwaka katika viwanja vya Lamore Jijini Tanga na yanashirikisha timu mbalimbali kutoka kwenye Jimbo la Tanga Mjini linaongozwa na Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya

“Leo nimekuja Tanga kwa lengo la kuja kuangalia viwango vya wachezaji ili baadae nimpiga simu kocha wa timu ya Taifa kuona namna nzuri ya kuweza kuwajumuisha kwenye timu zetu za Taifa”Alisema Waziri Ndumbaro.

Katika Fainali hiyo timu za Nguvumali na Kiomoni zilitinga hatua hiyo kwa kufanya vizuri kwa kila mmoja kumtoa mpinzani mwenzake na hivyo kulazimika kukutana kwenye hatua hiyo ya kumsaka Bingwa ambapo Bingwa alikuwa ni timu ya Kiomoni

“Kwa heshima ya Waziri Ummy Mwalimu nimeacha shughuli zote nimekuja Tanga mimi Waziri wa michezo ili niweze kuona vipaji vilivyopo hapa Tanga kwa maana historia ya mpira ni kubwa na nimeambiwa Juma Mgunda yupo hapa hivyo tunaweza kutumia mashindano haya kupata wachezaji wa timu ya Taifa”Alisema Waziri Ndumbaro.

Akubali Ombi la Mbunge Ummy

Katika hatua nyengine Waziri Ndumbaro amekubali ombi la Mbunge Ummy Mwalimu ambaye alimuomba atafute shule mmoja mkoani humo waifanye kuwa ya vipaji vya michezo.

Akijibu Ombi hilo Waziri Dkt Ndumbaro alisema kwamba yeye akisema wataona namna ya kwenda kulitekeleza ili uwepo wa shule hiyo uweze kupatikana mkoani Tanga.

“Mh Ummy nimepokea ombi lao wewe ukisema mimi ni utekelezaji tu hivyo nitakwenda kulifanyia kazi”Alisema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...