Na Janeth Raphael - MichuziTv -Dodoma


WAZIRI wa Madini Mh Anthony Peter Mavunde(mb) ametoa Rai kwa Wawekezaji wote nchini wenye leseni za uwekezaji katika sekta ya Madini kuzingatia sheria ya Madini,Sura ya 123.

Waziri Mavunde amesema wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akitoa Taarifa ya ya ukuaji wa sekta ya Madini Leo hii march 22/2024 Jijini Dodoma.

Na kuongeza kuwa Wizara ya Madini itatoa ushirikiano kwa wawekezaji wote wa ndani na nje ya nchi wenye nia ya kufanya uwekezaji wenye tija.

"Naomba nitoe Rai kwa wawekezaji wote wenye leseni za uwekezaji katika sekta ya Madini kuzingatia sheria ya Madini, Sura 123. Aidha Wizara ya Madini itaendelea kuwapa ushirukiano wawekezaji wote wa Madini ndanj na nje ya Nchi wenye nia kufanya uwekezaji wenye tija na kukuza uchumi wa Taifa letu kutikana na uvunaji rasilimali Madini "

Aidha Waziri ametoa angalizo la kusitishwa kwa akaunti za wamiliki wa uombaji na usimamizi wa leseni kwa njia ya mtandao ambao wameonesha matumizi mabaya ya mfumo huo kwa kuwasilisha maombi kwa lengo kuhodhi maeneo.

" Nachukua nafasi hii kutoa Taarifa kwa wamiliki wa maombi pamoja na leseni ambao wamekiuka au kutotekeleza sheria ya Madini,Sura ya 123,kuwa maombi na leseni husika zitafutwa ili kupisha waombaji wengine kupata fursa kuomba maeneo hayo".

"Aidha kwa wamiliki wa akaunti za uombaji na usimamizi wa leseni kwa njia ya mtandao ambao wameonesha matumizi mabaya ya mfumo huo kwa kuwasilisha maombi kwa lengo la kuhodhi maeneo bila kuendelea na taratibu za upatikanaji wa leseni akaunti zao zitasitishwa".

Ameongeza kuwa uchambuzi uliofanywa na Tume ya Madini umebaini kuwa hadi February 2024 jumla ya maombi 2,180 hayajalipiwa Ada stahiki na maombi 409 ambayo wamiliki wake wamelipia ada za maombi lakini hawajawasilisha nyaraka muhimu.

"Katika uchambuzi uliofanywa na Tume ya Madini imebainika kuwa hadi February 2024 kuna jumla ya maombi 2,180 ambayo hayajalipiwa ada stahiki za maombi . Aidha uchambuzi huo umebaini kuwa kuna watumiaji wa 5 wa mfumo wa uwasilishaji wa maombi kwa njia ya mtandao ambao wamekuwa wakitumia mfumk vibaya kwa kuwasilisha maombi bila kulipa ada stahiki".

"Vilevile katika uchambuzi uliofanywa na Tume ya Madini imebainika kuwa hadi February 2024 kuna uwepo wa maombi 409 ambayo wamiliki wake wamelipa ada za maombi lakini hawajawasilisha Nyaraka muhimu zinazoambatana na maombi hayo".

Leseni zilizotolewa na Tume ya Madini kati ya mwaka 2018 hadi 2024 ni.

2018 hadi 2019 leseni 5,094.
2019 hadi 2020 ni leseni 7,215.
2020 hadi 2021ni leseni 7,968.
2021 hadi 2022 ni leseni 9,498.
2022hadi 2023ni leseni9,642.
Na kuanzia 2023 hadi February 2024 ni leseni 8595.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...