NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maonesho ya biashara kwa wanawake wa masoko yatakayoendana sambamba na upimaji wa afya. 

Maonesho hayo ambayo yameandaliwa na Mfuko wa Udhamini wa Wanawake Tanzania (WFT) kwa kushirikiana na Taasisi ya Women TAPO pamoja na Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) yatafanyika katika Viwanja vya Mnazo Mmoja Jijini Dar Es Salaam katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 5, 2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa women TAPO Lulu Yassin amesema kuwa wamechagua kundi la wanawake wa masokoni kwa kuwa ndio kundi ambalo limeachwa nyuma kidogo katika harakati za ukombozi wa wanawake kiuchumi na kifikra.
 
Aidha amesema adhima yao kuu ni kuleta ufanisi katika maisha ya wanawake kwa kuhakikisha suala la usawa wa kijinsia katika masoko linatiliwa mkazo kuwakomboa kutoka hali duni.

"Malengo yetu makubwa ni pamoja na uwezeshaji wa wanawake wa masokoni kiuchumi,uinuaji ujuzi wa katika masuala ya ujasiriamali,utetezi na ufahamu wa sheria,haki, Uongozi,rushwa ya ngono,usawa wa kijinsia na ujenzi wa nguvu za pamoja kwa wanawake"
Amesema.

Kwa upande wake Mratibu wa masuala ya kijamii kutoka MEWATA, Dkt. Aha Mahita ameipongeza taasisi ya WOMEN TAPO kuwaalika katika maadhimisho hayo ambapo itakuwa fursa ya kuwahamasisha wanawake kupima saratani ya mlango wa  kizazi ambayo imeleta athari kwa zaidi ya asilimia 25.

Naye Mfanyabiashara Soko la Tabata Mission Bi.Maria Ismail ameishukuru taasisi ya WOMEN TAPO kwa kumpatia mafunzo mbalimbali ambayo yamemsaidia kujiamini,na kubuni bidhaa mbalimbali  kama mjasiriamali ambapo imemuinua kiuchumi nakuondokana na hali ya kuwa tegemezi.
 
"Nashukuru sana uongozi wa Women TAPO umenitoa nilipokuwa hadi hapa nilipo, nimepata mafundisho ya  ujasiriamali na kuwa jasiri, hapa nilipo naweza kugombea uongozi, nina uwezo wa kukaa bungeni nikatoa hoja zangu na nikasikilizwa". Amesema Bi. Maria

Maadhimisho hayo yatafanyika Machi 07,2024, yatambatana na matembezi ya amani kuangazia maisha ya wanawake wa masokoni kutokea soko la Kisutu hadi viwanja vya Mnazi Mmoja na pia kutakuwa na upimaji wa afya bure kwa kinamama na vilevile mafunzo ya ujasiriamali na fedha yatatolewa na wataalamu wa masuala ya kifedha.













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...