Liquid Intelligent Technologies (Liquid), sehemu ya Cassava Technologies, kampuni ya teknolojia iliyopo Afrika nzima inayofanya shughuli zake nchini Tanzania, imejizatiti kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa kitovu cha teknolojia kwa Afrika Mashariki kwa kutoa huduma za ubora wa hali ya juu kupitia uboreshaji endelevu ili kuwanufaisha wateja nchini kote.

Hayo yamebainisha baada ya kampuni hii kutunukiwa tuzo mbili za heshima zilizoandaliwa na Taasisi ya Usimamizi wa Wateja zilizotolewa mwanzoni mwa mwaka huu jijini Dar es Salaam.

“Kwa makadirio ya ukuaji wa Pato la Taifa kwa asilimia 6.3 mwaka 2024, Tanzania inapitia mabadiliko ya kidijitali ambayo ni ishara nzuri ya kukua zaidi kiuchumi. Tuzo hizi ni uthibitisho wa dira yetu ya kujenga Tanzania iliyounganishwa kidijitali ambayo haimwachi mtu nyuma.

Tunaamini kwamba ubora wa huduma ni sehemu muhimu ya safari hii, na tumejizatiti kuendelea kuboresha huduma zetu ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu yanayobadilika kila kukicha.

Tumefurahi kupokea tuzo hizi na tutahakikisha kuwa wateja wetu wanaendelea kupata huduma bora ya kiwango cha hali ya juu kuendana na chapa yetu,” alisema Manish Govindji, Mkurugenzi Mtendaji wa Liquid Intelligent Technologies Tanzania.

Katika tuzo hizo kampuni ya Liquid Tanzania ilishika nafasi ya tatu katika kipengele cha ‘Sekta Bora Katika Mawasiliano’, ikiwa ni mtoa huduma pekee wa huduma za intaneti katika tatu bora, ikisisitiza dhamira yake ya kutoa huduma bora za mtandao wa intaneti.

Mafanikio haya pia yanaangazia lengo la kampuni la kutoa huduma za kuaminika na suluhisho la kiubunifu kwa watu binafsi na wafanyabiashara nchini Tanzania. Pia ilishika nafasi ya pili katika kipengele cha 'Shirika Lililoboreshwa Zaidi', ikionyesha umakini wake katika ukuaji na ubora endelevu.

Upatikanaji wa mtandao wa intaneti wenye kasi ya hali ya juu na teknolojia za kidijitali ni muhimu ili kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa kitovu cha teknolojia kwa Afrika Mashariki, na Liquid imejizatiti kuleta ujumuishaji wa kidijitali kuwa uhalisia nchini kote.

Taasisi ya Usimamizi wa Wateja imekuwa ikiandaa Tuzo za Ubora wa Huduma katika nchi 11 duniani tangu mwaka 2010, zikiwemo nchi kadhaa za Afrika, na 2024 imefanikisha kushuhudia tuzo hizo zilifanyika Tanzania kwa mara ya kwanza.
Meneja wa Kitengo cha Mtandao na Usaidizi wa Uendeshaji wa Liquid Intelligent Technologies (Liquid), Afka Charles (katikati) akipokea cheti alichokabidhiwa baada ya kushinda tunzo za Annual Tanzania Service Excellence Awards 2024 zilizoandaliwa na Chartered Institute of Customer Management (CICM) mwanzoni mwa mwaka jijini Dar es Salaam huku akishuhudiwa na Mkurugenzi wa Biashara ya Kimataifa na Diplomasia ya Uchumi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi John Ulanga (kulia). Kampuni hiyo ilishika nafasi ya tatu katika kipengele cha ‘Sekta Bora Katika Mawasiliano’ na nafasi ya pili katika kipengele cha 'Shirika Lililoboreshwa Zaidi', ikionyesha umakini wake katika ukuaji na ubora endelevu.
Meneja wa Kitengo cha Mtandao na Usaidizi wa Uendeshaji wa Liquid Intelligent Technologies (Liquid), Afka Charles (kushoto) pamoja na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Neema Phiri (kulia) wakiwa wameshikilia vyeti walivyokabidhiwa baada ya kushinda tunzo za Annual Tanzania Service Excellence Awards 2024 zilizoandaliwa na Chartered Institute of Customer Management (CICM) mwanzoni mwa mwaka jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Biashara ya Kimataifa na Diplomasia ya Uchumi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi John Ulanga (kushoto) akikabidhi cheti kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Liquid Intelligent Technologies (Liquid), Neema Phiri (wa pili kushoto) baada ya kushinda tunzo za Annual Tanzania Service Excellence Awards 2024 zilizoandaliwa na Chartered Institute of Customer Management (CICM) mwanzoni mwa mwaka jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo ilishika nafasi ya tatu katika kipengele cha ‘Sekta Bora Katika Mawasiliano’ na nafasi ya pili katika kipengele cha 'Shirika Lililoboreshwa Zaidi', ikionyesha umakini wake katika ukuaji na ubora endelevu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...