Na Jane Edward, Arusha

Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa kumi wa wahasibu wa ndani kutoka ndani na nje ya nchi unaofanyika mkoani Arusha kwa muda wa wiki moja.

Akizungumza Mkoani Arusha na waandishi wa habari kuhusu mkutano huo ,Waziri wa fedha serikali ya mapinduzi Zanzibar ,Saada Mkuya amesema mkutano huo ni muhimu sana kwa wahasibu hao wa ndani kwani ndio wanaokagua maswala mbalimbali ya fedha kwa ukaribu.

Amesema ,kupitia mkutano huo watabadilishana uzoefu na mawazo namna gani kada hii ya maswala ya ndani yanavyoenda kutoka kwa wakaguzi nje ya nchi sambamba na kuangalia maswala ya utawala bora namna ambavyo wanafanya kazi.

Aidha wahasibu wa ndani wana majukumu makubwa zaidi ikiwemo kuangalia utaratibu za usimamizi wa maswala ya fedha na kazi kwa kila siku .

"Hii kada watu hawajaielewa vizuri wanataka kuhakikisha watu wanaofanya kazi kwenye hiyo kada wawe wanaielewa vizuri kada hiyo katika kujua nini cha kufanya na utaratibu wa kufuata na kuangalia namna bora ya utendaji kazi."amesema.

Pia amesema kuwa,wataweza kujadili namna ya utendaji kazi wao katika kushirikiana kwa pamoja na kubadilishana uzoefu kwani sasa hivi maswala yamebadilika sana hasa swala zima la usalama mitandaoni hivyo ni vizuri wakabadilishana uzoefu.

"Tunapozungumzia swala la ukaguzi wa ndani lazima iende sambamba na utawala bora katika kuhakikisha wanasimamia kikamilifu fedha zilizopo na kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu na sheria zilizopo.

"Unapotaka kuwa mwasibu lazima ufuate miiko iliyopo na wajaze fomu ya maadili ambayo wahasibu wanatakiwa kujaza kama ambavyo wananyaza viongozi wa umma ili wawe wanaishi vizuri wasipoteze fedha umma"amesema.

Zelia Njeza ni Rais wa Taasisi ya wakaguzi wa ndani Tanzania, ambapo anasema kuwa,mkutano huo utashirikisha viongozi mbalimbali pamoja na taasisi za umma kutoka Afrika ambapo kwa Afrika kuna nchi 27 ambao ni washiriki wa mkutano huo na jumla ya washiriki kutoka nje ni zaidi ya mia tatu hamsini pamoja na wakaguzi wa ndani elfu moja.

Amesema kuwa, wanategemea mkutano huo utaleta chachu ya utendaji kazi kwa viongozi hao ambapo watajikita zaidi katika kuangalia utendaji kazi wao na kuisaidia serikali katika utendaji kazi wao.

Aidha amesema kuwa,waliweza kupitia mchakato mzima na kuweza kushinda kuwa na mkutano huo hapa Tanzania ,wameona kuwa wakiwa na sauti moja kama wakaguzi wa ndani wa Afrika itasaidia wao kujiendesha wenyewe na kusonga mbele kutoka hapo walipo.

Hata hivyo malengo makubwa ni kujikita zaidi katika teknolojia na kuangalia namna teknolojia inaenda kwa kasi na watajadili mambo mbalimbali kuhusu ubadhirifu wa fedha na kupata uzoefu kutoka Afrika na mabara mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...