Na Michael Machela

TIMU ya mchezo wa Pool ya Snipers yenye makazi yake Mwenge Mpakani Kinondoni jijini Dar es Salaam imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano Pasaka yaliyojulikana kama “Star Park Easter Grand Open Pool Competitions 2024” kwa kuifunga timu ya Masti yenye makazi yake Posta Ilala jijini Dar es Salaam 13 – 8 na hivyo kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu shilingi milioni moja.

Mshindi wa pili ni timu ya Masti ambayo ilizawadiwa pesa taslimu shilingi laki tano.

Mshindi wa tatu katika mashindano hayo ni timu ya Skylight yenye makazi yake Kijichi Temeke jijini Dar es Salaam ambao walizawadiwa pesa taslimu shilingi laki moja na mshindi wa nne ni Shani Cinema na Morogoro ambao walizawadiwa shilingi elfu hamsini.

Mashindano hayo yalikuwa na mchezaji mmoja mmoja(Singles) ambapo Melkizedeck Amedeus kutoka timu ya Snipers aliibuka kuwa bingwa kwa kumfunga Seif Hamadi 7 – 5 na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu shilingi laki tano.

Seif Hamadi alichukuwa nafasi ya pili na hivyo kuzawadiwa shilingi laki mbili.

Mshindi wa tatu mchezaji mmoja mmoja ni Patrick Nyangusi ambaye alizawadiwa shilingi laki moka na mshindi wa nne ni Festo Yohana ambaye alizawadiwa shilingi elfu hamsini.
Meneja wa Kampasi ya TEWW-Morogoro Dkt. Honest Kipasika, akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Taarifa za Shule ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa SEQUIP-AEP mjini Morogoro tarehe 25 Machi, 2024
Baadhi ya waratibu wa Mradi wa maboresho ya Elimu ya Sekondari Kwa njia Mbadala wakifuatilia mada juu ya matumizi ya Mfumo wa Taarifa za Shule wakati wa warsha inayofanyika mjini Morogoro tarehe 25 hadi 29 Machi, 2024

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...