Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe.Daniel G. Chongolo ameshiriki katika ibada maalumu ya Kanisa la KKKT Jimbo la Tunduma ikiongozwa na Askofu Mkuu wa makanisa ya KKKT Tanzania Dkt. Alex Malasusa iliofanyika katika mji wa Tunduma sambamba na uzinduzi wa ukumbi wa kanisa hilo.
Akiongea katika hafla hiyo Chongoloa amesema mkoa wa Songwe ni moja kati ya mikoa mikubwa na inayosifika kwa kilimo lakini cha ajabu ni moja ya mikoa yenye changamoto ya lishe hivyo amemuomba askofu Malasusa kupitia kaanisa la KKKT Jimbo la Tunduma kuhakikisha wanahubiri pia lishe ili kunusuru Mkoa na janga la udumavu
Aidha pia mkuu wa mkoa alimueleza askofu na waumini walioshuhudia uzinduzi huo jambo lingine linausumbua mkoa wa Songwe ni tatizo la mimba za utotoni na ndoa za utotoni hivyo amewaomba waumini wa KKKT kuisaidia serikali katika kukemea vitendo hivyo na kushiriki katika Malezi Bora ya watoto wetu
Akimalizia hotuba yake Chongolo amekemea vitendo vya mauaji kukithiri ndani ya maeneo mbalimbali ya mkoa.
Kwa upande wake Askofu Malasusa amesema mkoa wa Songwe umempata mkuu wa mkoa mchapa kazi kweli na anayesikia ushauri hivyo ameomba waumini wamuombe ili kazi yake iweze kuwa rahisi na bila kusahau awe msaidizi mzuri wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani ambae amemuamini kumleta Songwe amsaidie
Askofu amesema yale yote yaliosemwa na RC Chongolo yote pia ni majukumu ya Kanisa hivyo amewaleza waumimi wa KKKT Tunduma kuwa suala la lishe na malezi ni moja ya majukumu ya Kanisa na ni sehemu ya kuheshimi uumbaji wa Mungu na kutukuza hivyo jukumu la malezi na lishe .
Pia Malasusa ameagiza kila baraza la wazee Jimbo la Tunduma KKKT wanapokutana wawe wanajadiliana juu ya lishe na malezi ya watoto
Akimalizia Malasusa amekea pia vitendo vya mauaji na kusema hata Mungu vitendo hivyo havimfurahishi na ni kumuingilia Mungu majukumu yake hivyo amewaomba waumini kumrudia Mungu na kufuata makatazo yake ndani ya Biblia
Mkuu wa Mkoa Chongolo amechangia kiasi cha shilingi Milioni moja kama mchango wake wa awali wa kukamilisha Ujenzi wa Ukumbi huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...