Na Janeth Raphael -MichuziTv -Dodoma

Imeelezwa kuwa wakati Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akiingia madarakani Machi 2021 kulikuwa na Majaji wa Rufani 16 na katika Uongozi wake hadi kufikia 03 Septemba 2023 idadi ya Majaji wa Rufani imeongezeka na kufikia 35 ikiwa ni zaidi ya asilimia 100.

Hayo yameelezwa leo hii April 5,2024 Jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof.Elisante Ole Gabriel katika mkutano wake na Wanahabari wakati akielezea mafaniko ya Muungano ya miaka 60 katika Mahakama ya Rufani.

Prof Ole Gabriel amesema kuwa ongezeko la Majaji wa Mahakama ya Rufani limeenda sambamba na uanzishwaji wa Masjala ndogo ya Mahakama ya Rufani Nchini.

"Wakati Tanzania ikiadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kumekuwepo na ongezeko la Majaji wa Rufani. Ongezeko la Majaji wa Mahakama ya Rufani limeenda sambamba na uanzishwaji wa Masjala ndogo ya Mahakama ya Rufani nchini".

"Wakati Mh.Dkt Samia Suluhu Hassan akiingia madarakani machi 2023 kulikuwa na Majaji wa rufani 16 na katika uongozi wake hadi kufikia 03 September 2023 idadi ya Majaji wa Rufani imeongezeka na kufikia 35 ikiwa ni zaidi ya asilimia 100".

Sambamba na hayo Prof Ole Gabriel ametumia nafasi hii kutoa wito kwa wananchi kuwa wakati tulionao ni bora sana kwa afya ya Muungano hivyo tuutumie vizuri kadili inavyowezekana.

"Nimalizie kwa kutoa wito mimi kama Kiongozi,Mwandamizi wa Mahakama na Mtanzania sio vibaya nikitoa wito kwa niaba ya Mahakama kutoa Wito kwa Watanzania kwamba wakatu na Mazingira tuliyonayo sasa ni bora mno kwa afya ya Muungano hivyo tuutumie vizuri kadili inavyowezekana".

Profesa hakuacha kusisitiza kuwa ipo Faida kubwa ya kuwa kwenye Muungano kuliko kutokuwa kwenye Muungano.

"Tunadhani kuna faida kubwa ya kuwa kwenye Muungano kuliko kutokuwa kwenye Muungano,kwahiyo kuna faida zaidi kuwa pamoja kwenye Muungano huu. Lakini weledi,uadilifu na uwajibikaji ni moja ya nguzo za Mahakama Muungano tukishajiisha hivi vitu itakuwa ni jambo la maana sana".

Mahakama ya Tanzania sasa imetumiza miaka 104,tangu kuanzishwa kwake hapo mwaka 1920.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...