Na Said Mwishehe, Michuzi TV

VIONGOZI wa Wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kwa jina la Machinga pamoja na viongozi wa waendesha bodaboda na bajaji wamempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kumteua CPA Amoss Makala kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho sambamba na timu makini aliyonayo.

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Dk. Samia juzi amenteua Makala kuwa katika nafasi hiyo akichukua nafasi iliyoachwa na Paul Makonda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Wengine waliteuliwa na Dk.Samia ni Jokate Mwegelo ambaye alikuwa Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi(UWT) ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho.

Wakati Salum Hapi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ,hivyo sekretarieti ya Chama hicho baada ya kupangwa kwa safu hiyo imekamilika.

Katika mapokezi yaliyofanyika leo katika Ofisi za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam mamia ya wana CCM wamejitokeza kuwapokea viongozi hao ambapo makundi mbalimbali yamepata nafasi ya kutoa salamu na wengi wamempongeza timu hiyo ambayo wanaamini itafanya kazi yake kwa maslahi mapana ya Chama hicho.

Akizungumza wakati wa mapokezi hayo Mwenyekiti wa Waendesha bodaboda na babaji  Said  Chenga amesema wanafurahia uteuzi uliofanywa na Mwenyekiti wa CCM

"Nimpongeze Makala,Mongela, Jokate na Hapi.Makala ukiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ulitufanya waendesha bodaboda tuwe huru na mpaka leo tunaendelea na shughuli zetu bila kusumbuliwa.

"Tunakumbua ulivyotupeleka Rwanda kwa ajili ya ziara ya mafunzo.Tunampongeza Rais Samia kwa kumteua Makala na timu yake,amesema na kusisitiza kuwa wao wataendelea kutoa kila aina ya ushirikiano kwa viongozi hao kwani wana Imani nao kubwa.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Machinga nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Machinga Mtaa wa Kariakoo Steven Lusinde amesema anampongeza Rais Samia wa kutupatia safu hiyo yenye kasi kiutendaji.

"Makala alipoondoka Dar es Salaam aliyenda Mwanza nimepokea simu nyingi kutoka kwa Machinga wa Mwanza wanamlilia kwa kuondoka.Sasa Machinga wa Dar es Salaam tunakukaribisha na tuko pamoja na wewe."


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...