WALIMU waaswa kuweka muda wa ziada kujiendeleza kielimu hasa katika fani ya Masomo ya tehama ili kuweza kuwafundisha wanafunzi Mashule kwa kisasa zaidi na kueneza somo la tehama na kuendana na mifumo mbalimbali .

Akizungumza wakati wa Mahafali ya walimu 65 waliopatiwa mafunzo ya Tehama yaliyoandaliwa na Rotary ya Dar es Salaam ikishirikiana na Taasisi ya tehama (DIT) Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni Teresia Kyala amesema Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo Walimu hao wa Shule za Msingi ili waweze kuendana na kasi ya Teknolojia.

"Klabu hii ambao ndio wafadhili wa mafunzo hayo Wanaunga mkono Serikali hasa kurahisisha matumizi ya tehama na kupitia mafunzo hayo waliyopewa kwa kata tano na shule 10 watasimamiwa ili kuona mafunzo hayo walivonufaika nayo kwa kutengeneza taarifa mbalimbali kwenye Vishikwambi vyao."

Hata hivyo amesema Serikali imejitahidi Kugawa Vishikwambi Kwa shule mbalimbali ili viwawezeshe kutumia teknolojia katika kuboresha elimu.

"Kuna mifumo mingi ambapo mwalimu anahitaji tehama kufahamu hayo kupitia kwenye kishkwambi badala yake itarahisisha walimu kutokwenda Stephen steshenari kuomba kufanyiwa kazi hizo badala yake watafanya wenyewe. "

Nae Meneja Mradi wa Mafunzo hayo Jackline Woiso ametoa pongezi kwa wakufunzi pamoja na wafaidika wa mafunzo hayo ambao ni walimu wa shule za Msingi kutoka wilaya ya Kinondoni.

Aidha,amesema Mafunzo hayo yatakuwa endelevu ili walimu hao waweze kupata mafunzo zaidi na kwa kina kwa hatua zingine zijazo.

Hata hivyo ameongeza kuwa Klabu hiyo ya Rotary dar imepewa ufadhili na Klabu ya Vacuva kukamilisha miradi mbalimbali ikiwemo kupanda miti,kugawa Madawati pamoja na kukamilisha ya azima ya kutoa Mafunzo ya Tehama.

Pia ametoa rai kwa wanufaika hao kutumia mafunzo hayo kwa tija na kuwapa elimu walimu wengine ambao hawakufika mafunzoni hapo.

Mmoja ya wafaidika wa Mafunzo hayo Mwalimu wa shule ya Twiga Devis Malegesi amesema hapo awali alikuwa anatumia kishkwambi hicho kwa matumizi mengine Kama kutazama filamu na Kufanya mawasiliano na watu mbili lakini baada ya kupata mafunzo hayo yameweza kugundua kuwa hata katika kazi zake za ualimu anaweza kutunga mitihani na kuandaa mazoezi ya maswali mbalimbali pamoja na kuandaa matokea kupitia Kwenye Kishkwambi hicho .
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...