Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa, amekagua mabanda ya Maonesho ya Sekta ya Ujenzi ambayo yanalenga kutoa elimu na huduma kuhusu kazi zinazofanywa na Wizara ya Ujenzi na Taasisi zake.

Maonesho hayo yanayotanyika kwa siku mbili katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma kuanzia leo Mei 27, 2024 hadi Mei, 28 mwaka huu.

Maonesho hayo yataambatana na uwasilishwaji ya makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2024/25 ambayo itasomwa Mei, 29 - 30, 2024 bungeni jijini Dodoma.

Katika maonesho hayo wabunge na wananchi watapata fursa ya kujifunza na kuzifahamu kwa ufasaha kazi zilizofanywa na tasisi zote zilizopo chini ya Wizara ya Ujenzi kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...