Mdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekabidhi kombe la ubingwa wa ligi hiyo kwa timu ya Kengold yenye maskani yake Wilayani Chunya, mkoani Mbeya ambayo ndiyo bingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa 2023/2024.

Hatua hiyo inatoa ruhusa kwa mabingwa hao kushiriki Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League) katika msimu ujao wa 2024/2025 ikiungana na timu nyingine ya Pamba FC kutoka jijini Mwanza.

Hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa huo ilifanyika jana katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam ikipambwa na mechi ya kirafiki kati ya bingwa huyo na timu ya Pamba FC mechi iliyoisha kwa timu hizo kutoka suluhu ya 1-1.

Mkurugenzi wa Biashara wa benki ya NBC Elvis Ndunguru alimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi kwenye tukio hilo lililopambwa na uwepo wa Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mbaraka Batunga likihushuhudiwa pia na mamia ya wapenda soka wakiwemo mashabiki waliosafiri kutoka mikoa ya Mbeya na Mwanza. Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) Bw Steven Mnguto alimuwakilisha Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia.

Akizungumza kwenye makabidhiano hayo, DC Batunga alisema pamoja na kuipongeza timu ya Kengold kwa kuibuka kinara wa ligi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa miongoni mwa timu shiriki, aliishukuru benki ya NBC kuwa mdhamini mkuu wa ligi hiyo akibainisha kuwa udhamini huo kwa kiasi kikubwa umechochea ushindani kwenye ligi hiyo hatua ambayo anaamini imesaidia kutoa washindi wenye sifa ya kushiriki ligu kuu ya NBC kwa sifa na vigezo vinavyotakiwa na wapenda soka.

“Udhamini wa NBC umewezesha kuongeza ushindani kwenye ligi hii na kuboresha soka letu. Leo hii sisi Wanachunya tunajivunia kuwa washindi wa ligi iliyokuwa na ubora kama tulioushuhudia na kupitia ushindani huo tunaamini tunakwenda kutoa changamoto haswa kwenye timu tutakazokutana nazo ligi kuu ya NBC. Baada ya ubingwa huu tunakwenda kujipanga kuanzia kikosi hadi benchi la ufundi ili kujiweka sawa zaidi kwa ajili ya Ligi Kuu ya NBC…tunawakaribisha sana Chunya,’’ alisema.

Kwa upande wake Ndunguru alisema benki hiyo inayodhamini ligi tatu muhimu hapa nchini, itaendelea kuboresha zaidi ligi hizo ili ziendelee kutoa matokeo chanya kulingana na malengo ya udhamini huo ikiwemo suala zima la kuzalisha ajira ambapo kwasasa jumla ya ajira 7,000 za moja kwa moja zimezalishwa kupitia udhamini huo.

“Tunawapongeza sana washiriki wote wa ligi ya Championship lakini kiupekee zaidi tunawapongeza Kengold kwa kuibuka washindi kwenye ligi hii. Pongezi zetu pia tunazielekeza Pamba FC kwa kuwa mshindi wa pili na hivyo nae pia anakwenda kushiriki Ligi kuu ya NBC msimu ujao…hongereni sana,’’ alisema Ndunguru huku akiongeza “Pamoja na soka, tumekuwa tukisadia michezo mingine kama gofu na riadha kupitia NBC Dodoma marathon. Nia yetu ya kusaidia sekta ya michezo hapa nchini ni thabiti na tutaendelea kusaidia,”

Akizungumzia ubingwa huo Nahodha wa Kengold Charles Masai pamoja na kuwashukuru wadau wote kwa jitihada zao zilizosaidia kufanikisha ubingwa huo akiwemo mdhamini huyo kwa kuandaa mazingira mazuri kwa timu zote shiriki, aliahidi kwa niaba ya wachezaji wenzake kuhakikisha wanajipanga vema ili waweze kutoa ushindani zaidi kwenye ligi kuu ya NBC msimu ujao.



Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) Bw Steven Mnguto (wa pili kushoto) akikabidhi kombe la Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) kwa nahodha wa timu ya Kengold Charles Masai baada ya timu hiyo kuwa bingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa 2023/2024. Hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa huo ilifanyika jana katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam ikipambwa na mechi ya kirafiki kati ya bingwa huyo na timu ya Pamba FC mechi iliyoisha kwa timu hizo kutoka suluhu ya 1-1. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mbaraka Batunga (Kulia), Mkurugenzi wa Biashara wa benki ya NBC Elvis Ndunguru (wa tatu kushoto) pamoja na maofisa wengine wa benki hiyo.



Mkurugenzi wa Biashara wa benki ya NBC Elvis Ndunguru (katikati) akimvalisha medali mmoja wa wacheza wa timu ya Kengold baada ya timu hiyo kuibuka vinara wa la Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship). Hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa huo ilifanyika jana katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam ikipambwa na mechi ya kirafiki kati ya bingwa huyo na timu ya Pamba FC mechi iliyoisha kwa timu hizo kutoka suluhu ya 1-1. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mbaraka Batunga (Kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) Bw Steven Mnguto (wa pili kulia)






Wachezaji wa Kengold, viongozi na wadau mbalimbali wakijipongeza baada ya timu hiyo kuibuka kinara wa la Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship). Hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa huo ilifanyika jana katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam ikipambwa na mechi ya kirafiki kati ya bingwa huyo na timu ya Pamba FC mechi iliyoisha kwa timu hizo kutoka suluhu ya 1-1.



Muonekano wa kombe lililokabidhiwa kwa timu ya Kengold kutoka kwa mdhamini wa Ligi hiyo benki ya NBC baada ya timu hiyo kuibuka kinara wa la Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship). Hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa huo ilifanyika jana katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam ikipambwa na mechi ya kirafiki kati ya bingwa huyo na timu ya Pamba FC mechi iliyoisha kwa timu hizo kutoka suluhu ya 1-1.



Mkurugenzi wa Biashara wa benki ya NBC Elvis Ndunguru (katikati) sambamba na maofisa wengine wa benki hiyo wakijipongeza wakati wa hafla ya kukabidhi kombe la Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) kwa mshindi wa ligi hiyo timu ya Kengold. Benki hiyo ni mdhamini mkuu wa ligi hiyo. Hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa huo ilifanyika jana katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam ikipambwa na mechi ya kirafiki kati ya bingwa huyo na timu ya Pamba FC mechi iliyoisha kwa timu hizo kutoka suluhu ya 1-1.



Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB), Almasi Kasongo (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya NBC wakati wa hafla ya kukabidhi kombe la Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) kwa mshindi wa ligi hiyo timu ya Kengold. Benki hiyo ni mdhamini mkuu wa ligi hiyo. Hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa huo ilifanyika jana katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam ikipambwa na mechi ya kirafiki kati ya bingwa huyo na timu ya Pamba FC mechi iliyoisha kwa timu hizo kutoka suluhu ya 1-1.


Kiikosi cha Kengold kilichocheza dhidi ya Pamba FC kwenye hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa iliyofanyika jana katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam ikipambwa na mechi ya kirafiki kati ya bingwa huyo na timu ya Pamba FC mechi iliyoisha kwa timu hizo kutoka suluhu ya 1-1.


Kiikosi cha Pamba FC kilichocheza dhidi ya Kengold kwenye hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa iliyofanyika jana katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam ikipambwa na mechi ya kirafiki kati ya bingwa huyo na timu ya Pamba FC mechi iliyoisha kwa timu hizo kutoka suluhu ya 1-1.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...